Kutoka kushoto ni naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh.Simon Msanjila, Mkuu wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Profesa Mark Mwandosya na mwenyeketi wa baraza la chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Profesa Penina Mrama kwa pamoja wakiwa katika maandamano kuelekea katika ukumbi wa nyerere kabla ya hafra kuanza.Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia Mh.Simon Msanjila akihutubia katika hafra hiyo ya mahafari ya nne ya chuo kikuu cha sayansi na teknolojia kilichopo mkoani mbeya,Mh.Msanjila amekipongeza chuo hicho kwa kuongeza baadhi ya mafunzo ikiwemo mafunzo ya ufindi na mafunzo ya sayansi ya kiafya kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa mkoani mbeya.Pia mh.Simon Msanjila ametoa wito kwa kila mtu mwenye uwezo wa kujifunsa mafunzo ya sayansi na teknolojia yatolewayo katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia kilichopo mkoani mbeya na kuwataka wahitimu kuzikimbilia fursa mbalimbali haswa katika harakati za kutafuta ajira. Baadhi ya wahitimu wa stashahada ya kawaida na stashahada ya kwanza katika fani mbalimbali za sayansi na teknolojia ambapo jumla ya wahitimi wote walio maliza kozi hiyo sayansi na teknolojia katika fani mbalimbali ni 804 ambapo idadi kubwa ni jinsia ya kime.Baadhi ya wahitimu sambamba na wageni waalikwa na wafanyakazi wa chuo hicho cha sayansi na teknolojia walio hudhuria hafra hiyo ya maafari ya nne yaliyo fanyika katika ukumbi wa nyerere uliopo chuoni hapo mkoani mbeya.PICHA NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.
No comments:
Post a Comment