Pilika pilika za Libeneke lako pendwa katika kuangazia maeneo mbalimbali ya mji mkuu Dodoma, Ilifurahishwa na matumizi mazuri ya uvaaji na uzingatiaji wa kofia ngumu yaani "Helmet" jinsi ambavyo madereva wengi wa vipando mbalimbali ikiwemo pikipiki na vyombo vinginevyo kama ambavyo kionekanavyo hicho hapo juu ikiwa dereva sanjari na msaidizi wake wote wakiwa wamevaa kofia zao kujikinga kuepukana na kujipa tahadhari juu ya Ajari.
Pichani ni Dereva wa Pikipiki maarufu kwa jina la Bodaboda akiwa na abiria wake wakikatiza baadhi ya Mitaa Mjini Dodoma huku juu wakiwa wamevalia Kofia ngumu yaani "Helmet" wote wawili kwenye kipando hicho.
Bodaboda wa Dodoma safi sanaa kwa kuzingatia sheria ya uvaaji "Helment"
Mambo safi Dodoma Mikoa mingine tuige hii kwa usalama wetu wenyewe.
PICHA NA MR.PENGO WA MMG
No comments:
Post a Comment