Sunday, September 25, 2016

MOBISOL YAKABIDHI MILIONI 3 NA KIKOMBE TIMU YA ZALAGOZA FC MSHINDI WA MOBISOL CUP MBEYA.

Kutoka Shoto ni muwakilishi wa Timu ya Zalagoza Fc akipokea Zawadi ya kombe kutoka kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Mh.David Mwasilindi Mara Baada ya timu hiyo kuibuka mshindi katika ligi ya Mobisol Cub ligi iliyo andaliwa na kusimamiwa na kampuni ya kuzalisha Nishati ya Umeme wa Jua Mobisol ambao kwa sasa wanahudumia mikoa 17 Tanzania Kusambaza nishati ya Umeme wa Jua na kwa yeyote atakaye hitaji taarifa zaidi kuhusu Mobisol anaweza kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja 0800 755 000 Bure.
Burudani ikitolewa na Vijana Wa Mobisol kampuni Inayozalisha umeme bora na wenyekiwango wakitoa burudani katika Fainali ya Mobisol Cup kwa mwaka huu iliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya Hivi karibuni.
Mchezaji wa Timu ya Mbeya City B akijiribu kuwatoka wachezaji wa Timu ya Zalagoza Fc waliopigilia uzi mweupe Katika Fainali ya Mobisol Cup ambapo Timu ya Zalagoza Fc Ilibuka Mshindi na kupewa KItita cha shilingi milioni tatu, Mshindi wa pili ni Mbeya City B ambao nao walilamba kitita cha shilingi Milioni Moja Ikifuatiwa na Mshindi wa Tatu Fellaly Fc ambao nao walichukuwa kitita cha Shilingi Laki Tano kama mshindi watatu kutoka katika Kampuni ya Kuzalisha nishati ya Umeme  Bora na Salama wa Jua Tanzania Mobisol.
Baadhi ya Kikosi kazi cha Timu ya Mobisol Katika Picha Ya Pamoja ambao waliwachapa Vilivyo Timu ya Wanahabari wa Meya Gori Tatu kwa Moja Katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

No comments: