Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mh..Paul William Mtima Akikata utepe katika Uzinduzi Wa kampuni ya Mobisol kwa nyanda za juu kusini hivi katibuni iliyopo Soweto Block "U" Jijini Mbeya, Mobisol ni kampuni yenye asili ya Ujerumani inayoongoza kwa kutengeneza, kusambaza na kuuza Mitambo Umeme wa Jua (Sola) iliyo salama kiafya na mazingira katika ubora wa hali ya juu, Ikiwa mbadala wa nishati isiyo salama kwa gharama nafuu kwa watu wa vipato vyote.Mobisol inaboresha maisha ya mtanzania kwa kumpatia Mteja mtambo wa sola pamoja na sababu ya yeye kutumia mtambo wa sola tukimaanisha Mobisol inampatia mteja TV inchi19 hadi 32, Redio, Taa kuanzia 4 hadi 20 pamoj na Tochi yakusomea lakini kupitia mitambo hiyo anaweza kutumia ving’amuzi, deki, sabwoofer pamoja na Jokofu la sola.
Mteja anaweza akapata mtambo wa sola Watt 80, Watt 120 na Watt 200 kwa kulipa pesa taslimu au kulipa kwa awamu ambapo atatoa kianzio cha shilingi 118,000/= Kisha atapewa Mtambo wa sola, Vifaa pamoja na fundi atake kwenda kufamfungia huo mtambo anataendelea kulipa kidogo kidogo kuanzia malipo ya siku hadi mwezi kulingana na kipato chake hadi pale atakapokuwa amekamilisha gharama za ununuzi huku kampuni ikibeba dhamana ya mtambo kwa kumpatia huduma za matengenezo au marekebisho ya kifaa kitakacho kuwa na tatizo bure katika kipindi cha miaka mitatu bure.
Kwakutambua na kupenda kuendelea kuenzi mahusiano mazuri na Wakazi wa Nyanda za juu kusini, Mobisol Mobisol ambao ndio wadhamini wakuu wa Ligi ya Mobisol Cup iliyoshika Kasi jijini Mbeya Ikihusisha Timu 20 Kutoka Mbeya Jiji, Mbeya Vijijini na Wilaya ya Chunya, Tarehe 13/08/2016 Ilifanya ufunguzi rasmi wa kuanza kufanya kazi Kanda ya nyanda za juu kusini uliofanyika Katika ofisi zao za kanda zilizopo Soweto Block C mkabala na jengo la sheli ya Oilcom. Na Kuhuduriwa na Viongozi mbalimbali wa Jiji la Mbeya huku Mkuu wa Wilaya Mbeya Jiji akiwa mgeni rasmi.Katika uzinduzi huu Mobisol walifanikiwa kufungua Duka kubwa na la kwanza Tanzania kwa ubora, Pia walifanikiwa kutambulisha na kuzindua Luninga (TV) ya sola ysa ukubwa wa nchi 32, TV ambayo ni kwanza kwa ukubwa Afrika Mashariki an Afrika kwa ujumla kuweza kuendeshwa na Sola.Katika kufanikisha lengo la kumpatia Mtanzania mkazi wa wa Mbeya na Nyanda za juu kusini Maisha Bora zaiidi kupitia uzinduzi huu Utaweza kushuhudia mradi bunifu tunaoendelea nao kwa kwasasa wa kutumia Ndege isiyo na rubani kuweza kumfikishia mteja huduma stahili kwa haraka na usalama zaidi.Mbali na kukupatia nafasi ya kuweza kushuhudia bidhaa zao pamoja na huduma za Mobisol, Mobisol walitumia tukio hili kama fursa ya kuweza kuonyesha na kujadili ni kwanamna gani Mobisoli imejipanga kuweza kutimiza dhamira ya kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwafikia watanzania wengi zaidi,ya 100000 Walio Kanda ya Nyanda za juu kusini. „Toka imeanzisha huduma zake Juni Mosi, Mkoani Mbeya Mobisol tumefanikiwa kuwanufaisha zaidi ya wakazi 900 Mkoani Mbeya katika hao Wanafunzi 400 wamepata muda wa ziada kujisomea kupitia mwanga unaozalishwa na mtambo ya Mobisol, Tumetoa Fursa za kibiashara kwa zaidi ya wakazi 50 Mkoani mbeya ambao wamefanikiwa kuanzisha biashara za kuchajisha simu, kufungua saluni za kunyoa nyoa nywele na kuonyesha Sinema, Kupitia program ya Mteja bingwa Kila mtumiajia wa Mtambo wa Mobisol anapewa fursa ya kumuunganisha ndugu jamaa rafiki na kujipatia Shilingi 15000/=.Zaidi kupitia Akademia ya Mobisol, tumetengeneza fursa za ajira kwa vijana mkoani Mbeya ambao hupewa mafunzo Maalum ya mamna ya kufanya Mauzo na Ufundi an mara baada ya kufuzu mafunzo na kuthibitishwa hupata fursa ya kufanya kazi na Mobisol kwa kuleta wateja, kuwafungia mtambo pamoja kuwahudumia wateja ikiwa ni sehemu ya dhamana inayotolewa na Mobisol kwa wateja wetu. Mpaka sasa tunafuraha kuajiri vijana zaidi ya 50 katika fani ya Ufundi, Masoko na Mauzo“ Hayo yaliongelewa na Meneja Masoko wa Mobisol Nyanda za Juu kusini Ndugu Lusajo Mwakapeje Latika uzinduzi huo aidha aliongeza kuwa kwa sasa wanahudumia mikoa 17 Tanzania na kwa yeyote atakaye hitaji taarifa zaidi kuhusu Mobisol anaweza kupiga simu kituo cha huduma kwa wateja 0800 755 000 Bure.
Mawasiliano kwa mteja Lusajo Mwakapeje
Marketing Team Leader-Southern Highlands zone
Mobisol Tanzania
Mob: +255652399348
Skype: sajo.tz
Mobisol UK Limited | Block "U" Mbeya Service Trade Soweto| 2013 Mbeya Tanzania.
Mob: +255652399348
Skype: sajo.tz
Mobisol UK Limited | Block "U" Mbeya Service Trade Soweto| 2013 Mbeya Tanzania.
Katika Taswia ni Mchezaji wa timu ya Ilemi Fc bwana Rajabu Jezi ya bluu bahari akijaribu kuwatoka wachezaji wa timu ya Msumari wa Moto katika mchezo ulio chezwa hivi karibuni katika viwanja vya shule ya msingi mwenge na kutoka sare ya bila kufungana ikiwa ni muendelezo wa ligi ya Mobisol inayo endelea hivi sasa mkoani mbeya kwa udhamini mkubwa wa Mobisol Mabingwa wa nishati ya umeme wa Jua "Sola" Tanzania.
No comments:
Post a Comment