Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili
kutoka kushoto) akizungumza na kundi la waandishi wa habari kutoka
nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo walipotembelea taasisi hiyo.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland
nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa masuala ya Ushirikiano
kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa Utafiti na Sera
kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu.
Kundi
la waandishi wa habari 15 kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi
ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja kati ya mafunzo yao katika programu
maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya
Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda wa siku tano pia
walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya
Finland.
Mratibu
wa programu ya Maliasili Bi. Namwaka Omari (kulia) akitoa mada kwa
waandishi hao wa habari kuhusu namna Taasisi ya UONGOZI inachangia
katika kuimarisha usimamizi wa maliasili zetu nchini hususan katika
sekta ya mafuta na gesi.
Mmoja
kati ya waandishi hao akiuliza swali. Baadhi ya mada zilizogusiwa
katika mazungumzo ni pamoja na jinsi gani Tanzania inatekeleza dhana ya
maendeleo endelevu, uimarishaji wa uwezo kwa viongozi barani Afrika,
uchumi wa sekta ya gesi nchini na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya
UONGOZI katika mazingira ya Serikali Mpya.
Mkuu
wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi.
Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno lake la shukrani kwa niaba ya
waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland,
walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli zake mapema leo.
No comments:
Post a Comment