Friday, March 11, 2016

TATOA KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA 12 MANISPAA YA TEMEKE.

Mwenyekiti wa wa chama cha wamiliki wa malori Tanzania (TATOA), Angelina Ngalula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ujenzi wa madarasa 12 katika manispaa ya Temeke.
Sehemu ya Bodi ya TATOA  na watendaji wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza na bodi ya TATOA jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA cha Wamiliki wa Malori nchini (TATOA) kinatarajia kujenga madarasa 12 katika shule msingi maji matitu ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono Rais Dk.John Pombe Magufuli ya kuhakikisha shule zinaboreshwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amesema kuwa wanatambua mchango wao na kuwa watakuwa wamesaidia jitihada za serikali katika kupunguza changamoto za madarasa.

Amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unakabiliwa na changamoto ya madarasa na madawati hivyo kunahitaji wadau kujitokeza kusaidia maeneo hayo.

Mwenyekiti wa TATOA, Angelina Ngalula amesema kuwa wameunga mkono jitihada za serikali kwa upande wa elimu hivyo wanawajibu wa kufanya hivyo katika kutatua changamoto ya vyumba vya madarasa.

Amesema kwa kuanzia wanaanza na madarasa 12 lakini wataendelea kuwasiliana na wanachama zaidi katika kuongeza au kujenga shule nzima ili watoto wasome shule na kuja kuweza kutumikia sekta ya usafirishaji.

Angelina amesema kuwa bodi yao iko imara katika kwenda na suala la shule za msingi ili watoto wapate elimu bora kutokana na mkakati wa Rais kutoa kipaumbele ya elimu ya nchini.

No comments: