Friday, March 4, 2016

KIVUKO CHA MV KILOMBERO II KUANZA KAZI.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

                     YAH:  KIVUKO CHA MV KILOMBERO II KUANZA KAZI.

WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuujulisha umma kuwa kivuko cha MV Kilombero II ambacho kilizama tarehe 27 Januari 2016, na kusababisha kusimama kwa hudum ya kivuko kwenye Mto Kilombero Mkoani Morogoro kimeanza kufanyakazi rasmi tarehe 29 Februari, 2016 mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.

Kivuko hicho kinaendelea na ratiba yake ya utoaji huduma ya kivuko kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 1:00 jioni kama kawaida.

Wizara inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza wakati kivuko hicho kikiwa kwenye matengenezo.
Taarifa hii imetolewa na                               
Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI),
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
04 Machi, 2016.

No comments: