Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ugobjwa wa Kisukari(Tanzania Diabets
Association), Profesa Andrea Swai akizungumza na waandishi wa habari
jinini Dar es Salaam leo kuhusiana na maradhi ya ugonjwa wa kisukari
pamoja na chanzo cha ugonjwa huo ambao sio wa kuambukizwa.
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ugonjwa wa Kisukari(Tanzania Diabets
Association), Profesa Andrea Swai katikati, kulia ni Mwathirika wa
ugonjwa wa Kisukari, Ramadhan Mongi na Mratibu wa Mpango wa kitaifa wa
kisukari Tanzania, John Gadna wakiwa katika mkutano na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kisukari.
CHAMA cha wagonjwa wa Kisukari Tanzania kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
kuandaa kambi ya upimaji wa ugonjwa wa kisukari bila malipo
Machi 13 katika viwanja vya shule ya msingi Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ugonjwa wa Kisukari(Tanzania Diabets
Association), Profesa Andrea Swai jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa
ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa ambao hauambukizwi ambao husababishwa na
ulaji mbaya.
Swai
amesema kuwa madaktari na matabibu watakuwepo kwaajili ya kupima afya
ya kinywa, kupima uzito naushauri wa lishe siku hiyo na
watakaogundulika matatizo maalumu watapewa rufaa.
Swai
amesema kuwa ugonjwa wa kisukari husababishwa na ulaji mbovu (kula
vyakula vilivyokobolewa), kutokufanya mazoezi na kutokula matunda.
Amesema
kila watu 100 wakikusanyika kwa kupima ugonjwa wa kisukari hapo
utawapata watu 9 wenye kisukari na 2 wanakuwa wanajua na wengine 7
hawajui kama wanaugonjwa huo.
Aidha ametoa wito kwa jamii kufuata kanuni bora za ulaji wa chakula ili kuepukana na ugonjwa huo usio wa kuambukizwa.
No comments:
Post a Comment