Tuesday, February 23, 2016

WAFUMBUZI WA MIFUMO YA TEKNOLOJIA KUNUFAIKA NA M-PESA.

 Mkuu wa kitengo cha mifumo ya kiteknolojia ya biashara wa Vodacom Tanzania, Josephat Kyando (kushoto)”Head of VAS & M-Commerce Technology” na Meneja wa huduma za M-Pesa wa kampuni hiyo, Polycarp Ndekana wakiangalia moja ya mifumo ya Kiteknolojia inayotumika kutoa huduma za kifedha wakati wa semina ya  siku moja ya wafumbuzi wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia  iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa makampuni binafsi ili kujua jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao jijini Dar es Salaam jana.

Baadhi ya wafumbuzi wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia  wa makampuni binafsi wakiwa kwenye semina ya  siku moja ya wafumbuzi wa mifumo hiyo  iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania ili kujua jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao jijini Dar es Salaam jana.

WAFUMBUZI wa mifumo mbalimbali ya Kiteknolojia  kutoka  makampuni binafsi jijini Dar es Salaam wamenufaika na mafunzo ya jinsi gani wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa kuboresha biashara zao katika Warsha  ya siku moja iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.

Akiongea kuhusiana na mafunzo hayo  Mkuu wa kitengo cha mifumo ya kiteknolojia ya biashara wa Vodacom Tanzania, Josephat Kyando alisema mafunzo haya   ni mafunzo ya kwanza bora yanayoendana na teknolojia ya kisasa ambayo hayajawahi kutokea hapa nchini yanayohusiana na huduma za M-Pesa ambayo kampuni imeanza kuyatoa sasa.

Kyando pia alisema kuwa washiriki wameweza kujua Programu za utekelezaji shughuli za kibiashara ambazo inaendelea kuzibuni na jinsi zitakavyotumika kuboresha uendeshaji wa biashara za sekta mbalimbali kupitia huduma ya M-Pesa.

“Hivi sasa huduma ya M-Pesa imekuwa na inaendelea kutumika katika huduma nyingi za malipo na kurahishisha biashara na kuwezesha watumiaji wake kuwa  na usalama wa maisha yao na fedha zao hivyo ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kukutana na wadau mbalimbali na kuwaelimisha ni kwa jinsi gani wataboresha biashara zao kupitia huduma hii”.Alisema.

Alisema kuwa makampuni mengi binafsi hususani yanayomilikiwa na kuongozwa na vijana wameonyesha mwamko mkubwa wa kuhudhuria mafunzo haya ambapo pia wanapata fursa ya kutoa maoni yao kuhusiana na jinsi unavyoweza kuboreshwa zaidi.

Katika semina hiyo ilibainishwa kuwa huduma ya M-Pesa inaweza kurahisisha na kuyapunguzia gharama wafanyabiashara na taasisi mbalimbali  katika kulipa mishahara ambapo badala ya kutumia muda mrefu kwenda kwenye mabenki wakawa wanalipwa kwa kutumia huduma hii ambayo inaongoza kuwa na watumiaji wengi nchini.

Kyando alisema kuwa Vodacom kupitia kampeni yake ya Life is Better imedhamiria kubuni huduma mbalimbali za kutumia mtandao kurahisisha maisha ya watanzania ikiwemo kuwapatia mawasiliano ya gharama nafuu.

No comments: