Wednesday, February 24, 2016

TUME YA MIPANGO YATEMEBELEA SHIRIKA LA MAENDELEO YA VIWANDA VIDOGOVIDOGO (SIDO)

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO), Omar Jumanne Bakari (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa timu ya wataalam kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Bibi. Florence Mwanri Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kuhusu ufanisi wa mashine ya kutengenezea sabuni katika kiwanda kidogo cha sabuni ambazo soko lake linapatikana jijini Dar es Saalam na mikoa ya jirani.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri (wa tatu kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Said Mjuli Mkurugenzi Mtendaji, kuhusu utengenezaji wa batiki katika moja ya viwanda vidogo vinavyofanya kazi chini ya mwamvuli wa SIDO. Wengine pamoja nae ni wataalam kutoka Tume ya Mipango na SIDO.
Kaimu Katibu Mtendaji,  Florence Mwanri pamoja na timu ya maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu Bw.George Buchafwe kuhusu utengenezaji wa mazulia kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.
 Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango  Florence Mwanri,(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Obedi Sylvester Musiba Mkurugenzi wa kampuni, (wa kwanza kushoto), kuhusu bidhaa wanazotengeneza kutokana na mimea na matunda. Wengine ni Bw. Omar Jumanne Bakari, Mkurugenzi Mkuu SIDO (wa pili kushoto), Bw. Omary Abdallah, Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Mipango na Ufuatiliaji (wa tatu kushoto), pamoja na maofisa kutoka Tume ya Mipango.
 Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Abdallah Kayumbi (wa kwanza kulia) kuhusu uzalishaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha nishati ya umeme kwa kutumia upepo (wind Turbines).
 Viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango na SIDO wakiangalia mashine ya kuzalisha nyuzi kwa ajili ya kutengeneza nguo inavyofanya kazi katika kiwanda cha Fruitful Goshen, Matengenezo Textile. 
 Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango,  Florence Mwanri alipata pia fursa ya kutembelea kiwanda cha TEMSO Engineering kinachozalisha vifaa mbalimbali vya ujenzi kama vile mashine za kufyatulia matofali na matoroli (wheelbarrows).
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Omar Jumanne Bakari, (aliyesimama), akitoa maelezo kwa viongozi na maofisa kutoka Tume ya Mipango (waliokaa kushoto) kuhusu SIDO inavyofanya kazi katika kuwasaidia wazawa ili kukuza uwekezaji katika viwanda vidogo vidogo. Waliokaa kulia ni wamiliki wa viwanda vidogovidogo wanaofanya shughuli zao chini ya SIDO. 
Na: Thomas Nyindo.
Tume ya Mipango.

No comments: