BENKI ya NMB imefungua rasmi tawi lake jipya wilayani Kakonko. Tawi hili limefunguliwa na mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali mstaafu Issa Machibya.
NMB Kakonko linakuwa miongoni mwa matawi zaidi ya 170 yaliyotapakaa nchini kote na katika kila wilaya bila kujali wilaya ipo pembezoni vipi. Tangu kubinafsishwa mwaka 2005, NMB imekuwa inaongeza matawi zaidi ya 10 kwa mwaka na hivyo kufikia matawi zaidi ya 170 mwaka huu.
Maono ya NMB ni kuhakikisha kuwa huduma za kibenki zinakuwa karibu zaidi ya wananchi na hivyo kuwaingiza watanzania kwenye uchumi rasmi kupitia huduma za kibenki kokote walipo hata kama ni wilaya za pembezoni mwa nchi.
Tawi la NMB Kakonko linatoa huduma zote za kibenki, ikiwa ni pamoja na huduma ya mikopo, kuweka na kutoa fedha, huduma ya fedha za kigeni, kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya malipo ya aina yoyote ambayo yanapatikana kwenye tawi lolote la NMB nchini.
Mbali na kufungua tawi la NMB Kakonko, NMB pia ilitoa msaada wa Madawati ya shilingi Milioni 5 kwaajili ya shule za msingi za wilayani hapo na pia vitanda vya hospitali kwaajili ya hospitali ya wilaya ya Kakonko vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 hivyo kufanya jumla ya msaada uliotolewa kuwa shilingi milioni 10.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma - Issa Machibya (wa tatu kutoka kushoto) aliyesimama pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kakonko – Toima Kiroya wakifungua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kakonko wilayani kakonko – Kogoma. NMB Kakonko ndilo benki pekee ililopo katika wilaya hiyo na ni tawi la nne kwa mkoa wa Kigoma. Wanaoshuhudia ni kutoka kulia ni Meneja wa Tawi - James Charles, Meneja Mwandamizi wa Mitandao ya Matawi ya NMB Taifa Gabriel Ole-Loibanguti na kulia ni Meneja wa Kanda ya Magharibi – Leon Ngowi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya akizungumza katika uzinduzi wa
uzinduzi rasmi wa Tawi la NMB Kakonko lililopo katika wilaya ya Kakonko – Kigoma.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya wa kwanza kulia akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi la NMB Kakonko lililopo katika wilaya ya Kakonko – Kigoma. NMB Kakonko ndiyo benki pekee ililopo katika wilaya hiyo na ni tawi la nne kwa mkoa wa Kigoma.Kutoka kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi – Leon Ngowi, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko – Toima Kiroya,Meneja wa NMB Kakonko – James Charles na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kakonko – Juma Maganga.
No comments:
Post a Comment