Ofisa Programu Dawati la Uangalizi wa Serikali wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Hussein Sengu (kulia) akitoa mada katika Kongamano la siku mbili la Wanawake Wafanyabiashara Sokoni Tanzania lililofanyika Dar es Salaam leo. Kongamano hilo lililowahusisha wanawake kutoka mikoa tisa ya Tanzania Bara limeandaliwa na Shirika la Equality for Growth (EfG)
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Japhet Makongo akizungumza na Wanawake wafanyabiashara waliohudhuria Kongamano hilo.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Sarah Mambea na Brenda Kharono.
Maofisa wa EfG, wakiwa kwenye Kongamano hilo, kutoka kulia Mussa Mlawa,Susan Sitta na Munaa Abdalah.
Wafanyabiashara wanawake Masokoni wakiwa kwenye Kongano hilo.
Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Tanzania (Repoa), Samwel Wangwe amewataka watanzania kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wanawake kwani wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa.
Akizunguza Dar es Salaam leo wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la kwanza la wanawake wafanyabiashara sokoni Tanzania, Wangwe alisema ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara hao wanawezeshwa na kuwajali katika uzalishaji na uendeshaji wa biashara zao.
Alisema kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa hali ya kiuchumi duniani katika sekta ya wafanyabiashara wadogo inaendelea kukua hivyo kutoa changamoto kubwa katika kuhakikisha inawekewa mazingira mazuri ya kisera.
"Wafanyabishara wadogo ni wengi sana hivyo wananafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa kutokana na uwepo wa asilimia 43 ya wajasiriamali wanawake Tanzania," alisema Wangwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wanawake wafanyabiashara walio sokoni kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa lengo la kuwajengea mshikamano na kujadili masuala muhimu yanayowahusu katika biashara zao.
Alisema kongamano hilo limehusisha wanawake 200 kutoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mtwara, Lindi, Mara, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, na mkoani Tanga katika Wilaya ya Lushoto huku wakiongozwa na kauli mbiu isemayo 'Sauti ya Mwanamke Sokoni'.
Alisema kauli hiyo inalenga kumkomboa mwanamke mfanyabiashara kwa kumjengea uwezo kutambua yeye ni nani na nafasi yake kama raia katika kuendesha shughuli biashara za shughuli za soko. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712-727062).
No comments:
Post a Comment