Mkurugenzi wa Global Publishers LTD, Shigongo Eric James (kulia), akishikilia vitabu vyake baada ya kumpatia jukumu la uzinduzi huo Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Kampuni hiyo, Oscar Ndauka. Tukio hilo limefanyika mapema leo ndani ya jengo la ofisi za GlobalPublishers zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia), akiwa amenyanyua moja ya vitabu hivyo baada ya zoezi la kukata utepe wa uzinduzi kukamilika. Katikati ni mtunzi wa kitabu hicho, Shigongo Eric James na Oscar Ndauka, wote wakiwa wamenyanyua vitabu hivyo. Vitabu vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni ’26 Secrets – How to Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Shigongo akimkabidhi jukumu la kukata utepe Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa Oscar Ndauka (wa kwanza kushoto) huku Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Abdallah Mrisho anashuhudia zoezi hilo.
Shigongo akiwaonyesha mojawapo ya vitabu hivyo baadhi ya wanahabari waliokuwa wakifuatilia kwa makini uzinduzi huo (hawapo pichani).
Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akiwakaribisha wanahabari katika uzinduzi huo.
Afisa Masoko wa Global Publishers Ltd, Benjamin Mwanambuu, akiongea jambo na waandishi wa habari kabla ya zoezi la uzinduzi huo kuanza.
Shigongo akisaini moja ya vitabu hivyo tayari ya kukitoa kama zawadi kwa baadhi ya wanahabari walioshuhudia uzinduzi huo.
MHAMASISHAJI na mjasiriamali wa kimataifa, Eric James Shigongo, amewaasa Watanzania kutokata tamaa katika kufuatilia ndoto zao huku wakiamini kuwa wao ni watu muhimu katika maisha yao na ya jamii.SOMA ZAIDI HAPA.
No comments:
Post a Comment