Thursday, May 28, 2015

TEMEKE YAKABIDHI MWENGE WA UHURU WILAYA YA ILALA SHAMRASHAMRA ZAPAMBA MOTO.

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi baada ya kumaliza mbio zake wilayani Temeke Dar es Salaam leo asubuhi. Mwenge huo umeanza mbio zake wilayani Ilala leo na kesho utakabidhiwa wilaya ya Kinondoni.
 Vijana wa hamasa wa wilaya ya Ilala wakishangilia katika hafla hiyo ya kukabidhiwa mwenge huo.
 Wananchi wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Vijana wa hamasa wakiimba nyimbo mbalimbali za mwenge.
 Wasanii wakitoa burudani.
 Mwenge ukiwasiri Kata ya Ukonga tayari kwa kukimbizwa wilaya ya Ilala.
 Kijana wa Skauti, Abuu Selemani akimvika skafu Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Juma Chum.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiwa amebeba mwenge wa Uhuru kabla ya kuanza kukimbizwa katika wilaya yake.
Watoto wa halaiki wakiimba wimbo maalumu wa mwenge. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments: