Kamanda wa Majeshi ya Anga wa Jamuhuri ya Botswana Meja General Mashinyana akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake waliotoka nje ya Tanzania kutokana na ukarimu walioupata Zanzibar wakati wa Mkutano wao wa Sadc – Sac.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika SADC – SAC uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mzizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC – SAC mara baada ya kuufunga Mkutano wao Zanzibar Beach Resort.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Majeshi ya Anga pamoja na washiriki wa Mkutano wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC – SAC mara baada ya kuufunga Mkutano huo Zanzibar Beach Resort.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Wakuu wa Majeshi ya Anga pamoja na washiriki wa Mkutano wa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC – SAC mara baada ya kuufunga Mkutano huo Zanzibar Beach Resort. Picha na OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Ushirikiano wa karibu unaozijumuisha Nchi za Jumuiya ya Mataifa ya Ukanda wa Kusini mwa Bara la Afrika SADC katika masuala ya Ulinzi wa Anga umesaidia kudhibiti changamoto za Amani na Usalama ndani ya ukanda huo. SOMA ZAIDI HAPA.
No comments:
Post a Comment