Monday, May 25, 2015

JESHI LA POLISI TANZANIA LAKABIDHIWA MASHINE ZA KUWEKA ALAMA SILAHA.

Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi, mashine 2 za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia Kituo hicho chenye Makao Makuu yake Jijini Nairobi. Halfa hii ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RESCA), Bw. Theoneste Mutsindashyaka (kulia) akitoa maelezo jinsi mashine za kuweka alama silaha zinavyofanya kazi. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu.
Mashine za kuweka alama silaha, zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania. Uwekaji wa alama katika silaha utasaidia udhibiti wa matumizi ya silaha hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe kushukuru msaada wa mashine zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya kuweka alama silaha.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IJP Ernest Mangu akishukuru kuhusu msaada wa mashine za kuweka alama silaha zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwa Jeshi la Polisi Tanzania katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam. Waliokaa toka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo, Bw. Theoneste Mutsindashyaka.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wa nne kutoka kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IJP Ernest Mangu (wa tatu toka kulia) na Katibu Mtendaji wa Kituo cha Kikanda cha kushughulikia Silaha Ndogondogo (RECSA) Bw. Theoneste Mutsindashyaka (wa nne toka kushoto) baada ya hafla ya kupokea mashine za kuweka alama silaha iliyofanyika katika Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Wengine ni Viongozi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu na wageni wengine waalikwa.

No comments: