Monday, May 11, 2015

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYANI HAI

Meneaja wa NMB kanda ya kasakazini Vicky Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa wilya ya Hai,Anthony Mtaka huku zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe.
DC Mtaka,Mbunge Mbowe na Meneaja wa NMB ,Bishubo wakifurahia msaada huo.
Msaada mwingine uliotolewa ulikuwa ni wa Blankets.
Chakula pia kilitolewa kwa wahnga hao.
Meneaja wa NMB,Vicky Bishubo akiwa na wahanga wa mafuriko .
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni ukanda wa chini wilayani Hai.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Benki ya NMB imetoa msaada  wa kibinadamu wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 baada ya kutembelea  eneo la tukio na kujionea athari kubwa zilizosababishwa na mafuriko hayo.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo,alitoa pole kwa familia zilizofikwa na kadhia hiyo huku akisema NMB imeguswa na tukio hilo na kwamba inatoa msaada katika maeneo matatu.

Alisema eneo la kwanza la msaada ni chakula ambapo imetoa unga kilo 
2,000,Maharage Kilo 500,Sukari Kilo 500 na mafuta ya kula lita 1,000.

Eneo jingine ni eneo la malazi ambapo yametolewa Magondoro 70,Mablangeti 100,pamoja na marobota ya nguo huku pia Benki hiyo ikichangia mifuko 50 ya Sementi kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Elerai iliyofikwa pia na mafuriko.

“Tumesikitishwa na majanga yaliowakuta,NMB tumekuwa na desturi ya kurudisha faida yetu katika jamii kwa kusaidia majanga mbalimbali hivyo tumetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 10”alisema Bishubo

Nao baadhi ya wahanga wa mafuriko hayo waliishukuru NMB kwa msaada huo na kutoa rai kwa watu,mashirika na taasisi mbalimbali zilizo za kiserikali na zisizo za serikali kuona umuhimu wa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu kutoka na adhari ziliwakumba.

No comments: