Baadhi ya vijana wanaofanya utapeli kwa kutumia vipande vya sabuni wakikimbia baada ya kunaswa na kamera ya bloger wetu wakiwa katika jitihada za kumwibia mmoja wapita njia katika mtaa wa Uhuru Dar es Salaam leo asubuhi.
Kwa Mujibu wa shuhuda vijana hao huwa kundi na baadhi huangalia mwenzao akitekeleza uhalifu wakati wao wakihakikisha wanampa ishara ya kufuatiliwa na kutoa ishara waonapo mazingira ya mchakato kushindikana ama hali kuwa tete kwa mwenzao iwapo mnunuzi wa simu atakuwa ameshtukia njama zao mbovu za kutaka kutenda uhalifu.
Mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam alikumbwa na mkasa wa kuibiwa shilingi laki moja alivutiwa na mhalifu mmoja kwa kumwonesha simu yenye gharama ya sh 200,000 huku akimsihi anunue kwa sh 100,000.
Alipokubali kununua simu hiyo, walimbadilishia wakati akitoa hela na alipoikabidhi na kwenda hatua chache aligundua kuwa amepewa kipande cha sabuni kwenye bahasha wakati mhalifu huyo na wenzake wameshatokea kusikojulikana.
Jambo la kusikitisha ni kwamba askari polisi wameshapokea malamiko ya mikasa kama hiyo lakini hakuna jitihada za makusudi zilizochukuliwa kuwanasa na kuwatia hatiani wahalifu hao.Tahadhari inatolewa kwa wananchi kutonunua bidha kama hizo mkononi kwa watu hasa katika mazingira ya ushawishi mkubwa na kufanya manunuzi kwenye maduka yenye kutoa risiti kwa bidhaa walizonunua. |
No comments:
Post a Comment