Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kiwanda cha Mbeya kimeeleza mafanikio muhimu ya kiwanda ambacho ni mojawapo ya Viwanda vinavyofanya vizuri zaidi Afrika na Dunia kwa ujumla, Katika ziara ya Waandishi na Wahariri wa vyombo mbalimbali Nchini walipotembelea kiwanda hicho Jijini Mbeya walipata kushuhudia namna ambavyo uzalishaji wa vileo mbalimbali kutoka katika kampuni ya Bia (TBL) Tanzania kuanzia mwanzo wa matayarisho yake mpaka hatua ya mwisho.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Imezungumza mengi na baadhi ya Waandishi kutoka vymbo mbalimbali nchini juu ya maendeleo ya Kiwanda kwa sasa na kipindi cha nyuma hali jinsi ilivyo kuwa na kuonekana kuwa kwa sasa kampuni hiyo inafanya vizuri zaidi kulinganisha na miaka mitatu iliyopita, Kulingana na jitihada mbalimbali na uchapakazi mahiri wa Kiwanda hicho kimebahatika kupata Tuzo mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kiwanda cha Mbeya kimeendelea kuwajali wafanyakazi na wateja kuanzia kiwandani mpaka sokoni na kuendelea kufanya vizuri Nchini kwa kuzalisha Bia zenye ubora na kiwango cha hali ya juu.
Mkurugenzi wa uzalishaji wa kampuni ya Bia nchini (TBL) Bwana Richmond Raymond Akielezea namna ambavyo kwa sasa kampuni inazalisha Bia kwa kiwango na ubora wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment