All Right Receved by MR.PENGO 2016

Monday, July 11, 2016

MISS MBEYA 2016 ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA AMANI NSALAGA JIJINI MBEYA...

Miss Mbeya 2016 Eunice Robert amewatembelea watoto yatima katika kituo cha Amani Nsalaga  Uyole mkoani Mbeya Hivi kalibuni na kuchangia baadhi ya mahitaji katika kituo hicho ikiwemo mchele, unga, sabuni,  mafuta yakupikia, nguo, vitenge, daftari, kalamu na mafuta yakupaka.    Aidha Miss huyo kutoka chuo kikuu cha Teofilo Kisanji ambaye ndiye anayeshikiria Taji la Umiss kwa sasa kwa Mkoa wa Mbeya amewaomba watu Binafsi, Mashirika ya Kidini, na Viongozi Mbalimbali wawe na mazoea ya kuwatembelea watoto yatima,  Wazee, Watu wasio jiweza, Wagonjwa na wale waliopo katika Mazingiza magumu na kuwasaidia kwa kuwa Jamii hiyo inahitaji Msaada kwa kiasi kikubwa hivyo sote tuguswe na hili.PICHA NA ECKY THE BEST MMG MBEYA.  Miss Mbeya 2016 Eunice Robert akiwa na baadhi ya Watoto kutoka katika Kituo cha kulelea Watoto Yatima Amani kilichopo eneo la Nsalaga Jijini Mbeya.Pia Miss Mbeya alishiriki Michezo mbalimbali na watoto wa Amani.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Post a Comment