Thursday, March 17, 2016

WAMILIKI WA MADUKA YA DAWA YALIYOKUTWA NA DAWA ZA SERIKALI WAFIKISHWE MARA MOJA MAHAKAMANI-DK.KIGWANGALLA.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangalla akizungumza katika mkutano wa matokeo ya ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangalla akiangalia baadhi ya vifaa tiba na dawa zilizo kamatwa katika operesheni hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
 NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto,  Dk.Hamis Kigwangallaameagiza Baraza la Wafamasia pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),kuwafikisha mahakamani wale wote waliokutwa na dawa za serikali katika maduka yao.

Kigwangalla  ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam baada ya kupewa matokeo ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa muhimu na yasiokuwa na vibali iliyofanywa na Baraza la Wafamasia na TFDA  pamoja na Jeshi la Polisi, amesema dawa zilizokamatwa zitaifishwe na kupeleka katika hospitali za serikali.

Amesema kuwa haiwezekani wananchi wakakosa dawa za serikali na kuonekana katika maduka ya dawa na watu hao wakaachwa bila kuchukuliwa hatua.

Kigwangalla amesema kuwa katika operesheni hiyo baadhi ya maduka yanauza dawa ambazo haziko kwenye orodha za dawa ikiwemo ni dawa ya usingizi ambayo inatakiwa kutumika wakati wa operesheni.

Aidha amesema kuwa baadhi ya maduka mengine yamefungwa lakini yanauza dawa nyakati za usiku na kuwataka wanaofanya operesheni kuendelea na wataokutwa wachukuliwe hatua mara moja.
Operesheni hiyo ilianza machi 1 hadi 3 mwaka huu ambapo walikagua maduka 685 katika mikoa tisa na kati hayo maduka 432 yamefungiwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo na kuwa na dawa za serikali pamoja na kuwa dawa za asili.

Aidha Kigwangalla amesema kuwa dawa ni sumu hivyo inatakiwa kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na wanaouza dawa ambazo hawana orodha nazo wanazalisha matatizo ya kiafya kwa wananchi.

Kigwangalla amesema hadi sasa ni dawa 65 tu ndiyo zenye nembo ya serikali na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapopata dawa serikali katika duka la dawa.

Amesema kuwa jeshi la polisi lichukue hatua ya kuwabana wale wote  waliokutwa na dawa za serikali kuwabana katika kuweza kuwapata waliokuwa wakiwapa dawa hizo.

No comments: