Tuesday, March 1, 2016

SADC YAJADILI UWEKEZAJI KATIKA SEKTA VIWANDA JIJINI DAR LEO.

 Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Julieth Kairuki akizungumza katika mkutano wa SADC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wawakilishi wa nchi mwanachama wa SADC wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji (TIC), Julieth Kairuki akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa wadau wa SADC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
SERIKALI imesema itaendelea kuboresha miundombinu ili kuweza kuvutia uwekezaji wa viwanda ili nchi iweze kukua kiuchumi.

Hayo ameyasema leo Katibu Mkuu wa Biashara na Uwekezaji, Adolff Mkenda katika Mkutano wa w tano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC),amesema kuwa katika kuhamasisha uwekezaji wa ndani nje serikali imejikita katika kujenga miundombinu ya barabara.

Amesema kuwa uchumi unakua kwa asilimia saba na nguvu kazi kubwa iko vijiji kwa theluthi mbili hivyo lazima kuweka mazingira uwekezaji katika nguvu kazi hiyo.

Mkenda amesema wakati inaanzishwa SADC ikiwa ni kujikomboa kisiasa lakini kwa sasa ni nchi kujikomboa katika uchumi katika sekta ya viwanda.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC),Julieth Kairuki amesema kuwa mkutano huo kufanyika nchini mafanikio ya kujifunza kwa nchi zingine zinavyofanya uwekezaji.

Amesema nchi 14 ziko nchini ambapo zitaweza kukubaliana ukuzaji wa uwekezaji wa viwanda katika mapinduzi ya kiuchumi kwa nchi zilizo katika jumuiya hiyo.

Julieth amesema TIC imeweka mazingira ya mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje na sio kugawa maeneo ya vijiji kwa wawekezaji huku wakiwa na hekta 122000.

No comments: