All Right Receved by MR.PENGO 2016

Monday, March 7, 2016

KAMPUNI YA KAZI SERVICES NA TEA WASHIRIKI KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KESHO KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR.


Mkurugenzi wa kampuni ya Kazi Service Ltd , Zuhura Muro (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani itakayofanyika kesho katika hoteli ya Serena jijini. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano katika shirika la nyumba Tanzania, Suzan Omary kulia ni Mkurugenzi wa ATE, Lilian Machela.

KAMPUNI ya Kazi Service Ltd kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kupitia programu ya Mwanamke wa Wakati ujao (Female Future) kuadhimisha siku ya wanawake duniani katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kesho kuanzia majira saa tisa na nusu alasiri.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Kazi Service Ltd , Zuhura wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani itakayofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kesho.

Zuhura amesema kuwa Siku hiyo yenye Kauli mbiu 'Kumuwezesha Mwanamke ili kupata usawa wa Kijinsia'.Pia siku hiyo itatumika kufurahia mafanikio ya mwanamke katika nyanja zote jamii,uchumi,utamaduni na siasa.

amesema kuwa Zaidi ya Wanawake 400 kutoka fani na idara mbalimbali kama vile watumishi wa Umma, Jeshi, Sheria na Sekta Binafsi watashiriki katika kuadhimisha siku hiyo Serena jijini Dar es Salaam.

Zuhura amesema kuwa mtoa maada katika maadhimisho hayo atakuwa Mrs. Petronella Joy Mwasandube , pia ameongeza kuwa 

maadhimisho hayo yatafanyika kwa namna ya kipekee ambapo kutakuwa na semina ya kuhamasisha maendeleo leo ya mwanamke.
Post a Comment