All Right Receved by MR.PENGO 2016

Saturday, February 6, 2016

MAHAFARI YA KUWATAMBUA MAFUNDI WALIOTOKA MTAANI NA UJUZI WAO KISHA KUPATA MAFUNZO RASMI NA CHUO CHA UFUNDI VETA YAFANA SANA JIJINI MBEYA....

Mgeni Rasmi wa Hafra hiyo Bwana Jastine Ruta Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi Veta kanda ya Mbeya akihutubia katika Hafra hiyo ya Wahitimu wa Mafunzo Rasmi ya Veta kwa walio kuwa na ujuzi katika Nyanja Mbalimbali ikiwemo Upishi, Uwashi, Ufundi wa Magari pamoja na Chakula na Vinywaji.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Veta kanda ya Mbeya Ndugu Lameck Padrii Kihinga akizungumza jambo katika Hafra hiyo ya Mahafari ya Mafunzo Rasmi yaliyo tolewa na Chuo cha Veta kwa Vijana na Watu Mbalimbali wenye Fani hizo za Ufundi kujiendeleza Kifani na kupata Cheti.
Baadhi ya wahitimu wakisoma Lisala kwa Mgeni Rasmi ikiwa ni miongoni mwakuhitaji Elimu ifike mpaka Vijijini juu ya ujasiliamali, Kujiajili au Kuajiliwa mara baada ya kuhakikiwa Kimafunzo, Mafunzo endelevu na kujiunga katika Vikundi Mbalimbali vya Ujasiliamali, Ubora wa kazi na Usalama, Kupata Mikopo na Sehemu Nzuri za kufanyia Mafunzo pia kusaidiwa Kutangaza shughuli zao katika Vyombo Mbalimbali vya Habari ikiwemo, Redio, Magaazeti, Vituo vya Terevisheni, Blog Mbalimbali Vipeperushi na Magari ya Matangazo.
Baadhi ya wahitimu wakiwa katika Ukumbi Mdogo wa Chuo cha Ufundi Veta iliyopo Ilomba Jijini Mbeya.


No comments: