All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, October 11, 2015

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA ABITAT JIJINI DAR ES SALAAM....

Ofisa Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mselem Mwanamsoga akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Sungura (kulia), wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. (Picha na Francis Dande).
 Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (wa pili kulia), na Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Mselem Mwanamsoga wakitoa maelezo kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, kwa watu waliofika katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. 
 Baadhi ya watu wakipata huduma katika banda la NSSF.
 Ofisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Aisha Sango (kulia), akigawa vipeperushi kwa watu waliotembelea banda la NSSF vyenye maelezo kuhusu huduma wanazotoa, ikiwemo uuzwaji wa viwanja vilivyopimwa katika eneo la Kiluvya, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wakati wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yaliyoandaliwa na Umoja wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki (Abitat), yanayoendelea katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Post a Comment