Wednesday, October 7, 2015

MSEMAJI WA SERIKALI: UTEUZI WA WAKUU WAPYA WA WILAYA ULIOFANYWA NA RAIS ULIZINGATIA SHERIA,KANUNI NA TARATIBU.......

mwambene
Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (kulia) akionesha kitabu cha Katiba ya Tanzania kifungu kinachompa mamlaka Rais kufanya uteuzi ilikuboresha Serikali yake awapo madarakani. kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Vicent Tiganya. Mkutano huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale.
DAR ES SALAAM Kufuatia vyombo vya habari nchini kuripoti taarifa kuhusiana na uteuzi wa Rais wa Wakuu wapya wa Wilaya uliofanyika hivi k aribuni, baadhi ya vyombo hivyo vya habari ikiwemo moja ya gazeti la kila siku nchini kuripoti kuwa uteuzi huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya kulipa fadhila na umetokana na masuala ya kisiasa na ni ufujaji wa wa fedha za umma. Hata hivyo Serikali imetolea ufafanuzi wa suala hilo kupitia Msemaji mkuu wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene amefafanua kuwa, Serikali imetimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu na Rais ana mamlaka ya kufanya uteuzi wakati wowote inapobidi kwa malengo ya kuboresha utendaji kazi Serikalini hivyo utezi huo wa Wakuu wa Wilaya ulizingatia vigezo vyote na taarifa hizo zilizoripotiwa na gazeti hilo ni za uzushi na za kupuuzwa.

“Serikali inapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya uliofanywa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 4/10/2015 ambapo jumla ya Wakuu hao wapya wa Wilaya 13 waliteuliwa na wengine Saba kuhamishwa vituo vua kazi. 

Hii ni kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu alizonazo Rais” alieleza Assah Mwambene katika ufafanuzi wake kwa vyombo vya habari.
Na kuongeza kuwa, taarifa hizo zilizoripotiwa ni za kichochezi na zinalenga kumchonganisha Mhe.Rais na wananchi wake.

Mkurugenzi ihuyo, aliongeza kuwa, Serikali inapenda kuvikumbusha vyombo vya habari kufanya utafiti kwa kusoma nyaraka mbalimbali kuhusu mamlaka ya Rais na kujiridhisha kama uteuzi huo umezingatia matakwa ya Katiba ya nchi au la.

“Aidha, tunaviomba vyombo vya habari kuandika habari zenye lengo la kujenga umoja na mshikamano badala ya kuandika habari zenye lengo la kuwagawa Watanzania.” Alimalizia Mkurugenzi huyo.

Mbali na kutolea ufafanuzi huo juu ya taarifa za uzushi, pia aliwataka wamiliki wa mitandao ya kijamii ikiwemo blog pamoja na wananchi wanaotumia mitandao hiyo ya kijamii kuweka taarifa zisizo za kweli na zinazopotosha umma, amewataka waache mara moja kwani Serikali inazifanyia kazi taarifa zote na muda wowote watachukuliwa hatua.

“Kumekuwa na taarifa za blog za habari kuweka habari za uongo na kuhaminisha watu habari zao hizo bila kufuata misingi na kanuni. Wapo walioripoti habari za uongo kwa kumsingizia kifo Waziri Abdala Kigoda kuwa amefariki dunia… huo ni uzushi na tumeendelea kukanusha kwa hilo pia kuna mtu alilipoti kuwa Mkuu wa Majeshi kunywesha sumu hilo nalo si la kweli huo wote ni uzushi unaoenezwa na watu kupitia blog na baadhi ya vyombo vya habari serikali itazichukulia sheria kali” amebainisha Mkurugenzi huyo.

Katika mkutano huo Assah Mwambene ametumia muda huo kuwataka waandishi kuzingatia wed=redi wa habari huku akiimiza kuchukua vitambulisho vya Serikali’Press Card’ kwani ndio vyenye dhamana ya kuwatambua katika weredi wao na utendaji makini katika kazi zao za kihabari.

“Mwandishi unatakiwa uwe na Press Card. Hii ni kama unavyoona leseni ya kibiashara kwa mfanyabiashara kuwa na leseni na mwandishi tunampatia leseni ambayo ni press card ambayo ndio inamfanya afanye kazi zake kwa uhuru” alimalizia Mkurugenzi huo.
mwa
Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (kulia) akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari
mwambene 3
muda wa maswali na majibu...
mwambene2Mkurugenzi Idara ya Habari, Assah Mwambene (kulia) na Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Vicent Tiganya, wakisikilza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari (Hawapo pichani). Mkutano huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.

No comments: