All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, August 30, 2015

MGOMBEA MWENZA SAMIAH SULUHU ANADI ILANI YA CCM MWAKA 2015 KATIKA KATA YA KYENGEGE,WILAYA YA IRAMBA....

Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa Chama cha Mapinduzi Bi.Samia Suluh akisalimiana na Mh;Mwigulu Nchemba ambaye ni mgombea Ubunge jimbo la Iramba hii leo,Bi.Samiah suluhu katika ziara yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Singida,hii leo amefika Kata ya Kyengege Jimbo la Iramba kwaajili ya kunadi Ilani ya CCM ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuomba kura za kishindo kwa nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais ifikapo Tar.25.10.2015
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mnec wa wilaya ya Iramba Ndg.Hasani Kilimba.Mshindi wa pili wa nafasi ya Viti maalum Mkoa wa Singida Bi.Martha Mrata akiimba wimbo wa "CCM ni Ile ile" kuashilia Ushindi upo pale pale kwasababu Watanzania bado wanaimani na Chama cha Mapinduzi.Bi.Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mshindi wa nafasi ya Ubunge- Viti maalum Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Kitaifa akimuombea kura Mgombea KURA MH;JOHN POMBE MAGUFULI  wa nafasi ya Urais kwa chama cha Mapinduzi Bi.Samiah Suluhu.Wakifurahia jambo baada ya Wanakyengege kuwahakikishia kuwa
CCM itashinda Jimbo la Iramba kwa asilimia 100.Mh;Mwigulu NChemba akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kyengege kuwa kwa sasa Tanzania inahitaji Rais Mchapa kazi na sio Muugizaji,Mbali na hilo Mwigulu Nchemba pia amewaomba wanairamba kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa nafasi ya Udiwani,Ubunge na Urais kwa CCM tu.Bi.Samiah Suluhu ambaye ni Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi akizungumza na Wananchi wa kata ya kyengege mambo mbalimbali anayodhamiria kuwafanyia mara baada ya kushinda hapo October 25.Kubwa amewaahidi kutatua kero ya Maji kwa Tanzania nzima ,Kujenga mabweni kwaajili ya watoto mashuleni,Kuinua Uchumi wa akina mama kupitia Mikopo mbalimbali na kupitia Utekelezaji wa Ilani ya CCM inayosema kila kijiji kimetengewa Milion 50 kwaajili ya maendeleo.Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Bi.Samiah Suluhu akimuombea Kura Mh;Mwigulu Nchemba kwa wananchi wa kata ya kyengege hii leo wakati wa mkutano wa kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.Kushoto ni Mgombea Ubunge jimbo la Mkalama kupitia CCM ambaye pia alihudhuria mkutano wa Kata ya Kyenge wilaya ya Iramba.Makamu wa Rais mtarajiwa wa Kwanza Mwanamke Nchi Tanzania akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Kyengege wilaya ya Iramba.Hapa akiwanadi washindi wa Ubunge Viti Maalum Mkowa wa Singida,Kushoto ni Ashyrose na Kulia ni Bi.Martha Mrata.
 Picha na Sanga Festo Jr.
Post a Comment