Wednesday, July 22, 2015

WANANCHI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAJITOKEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KWA MFUMO WA BVR...

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WANANCHI wa jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mfumo wa BVR lililoanza leo.

Wakizungumza na Globu ya Jamii kwa nyakati tofauti walisema zoezi linaenda vizuri lakini linakabiliwa na changamoto chache ambazo zikitatuliwa wananchi wote watajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura.

Akizungumzia suala kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ,Salumu Abbakari Mkazi wa Msisiri amesema kuwa alifika mapema na kuweza kujiandikisha lakini ameona kuna changamoto ya kituo kuzidiwa na watu.

Aidha amesema watu wasikilize maneno ya mtaani juu ya changamoto za kujiandikisha wafike na kuweza kujiandikisha wasikate tama wakati hawajafika eneo la tukio.

Abbakari amesema NEC wamejipanga vizuri kuandaa utaratibu lakini changamoto hazikwepeki baadhi ya kulalamika kutokana na kutokuwa wavumilivu wakiwemo vijana.

Nae Sophia Thomas amesema kuwa idadi ya waandikishaji iongezeke katika kuweza  kuondoa changamoto ya wananchi kukaa kwa muda mrefu.

Amesema changmoto zilizopo katika kituo haziwezi zikamfanya asijiandikishe kwani kura yake ni muhimu hivyo atajiandikisha na kuweza kupiga kura.
Wananchi wa Kata ya Mwananyamala wakiwa katika foleni  kujiandikisha katika Daftari la Kudumu Mpiga Kura katika mfumo wa alama za vidole (BVR), leo jijini Dar es Salaam.
 Mwananchi akiwa amekaa kwenye kiti kwa ajili ya kupiga picha ya kitambulisho cha kupigia kura katika zoezi kuandikisha wananchi Daftari la Wapiga kura kwa mfumo wa alama ya Vidole BVR katika Kituo cha Kujiandikishia cha Shule ya msingi Kambangwa  Wialya ya Kinondoni Jijini  Dar es Salaam.
 Wananchi wa Kata ya Mwananyamala wakiwa katika foleni  kujiandikisha katika Daftari la Kudumu Mpiga Kura katika mfumo wa wa alama za vidole (BVR)leo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC),akitoa taratibu za kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura kwa Mfumo wa kuchukua alama za Vidole katika Kituo cha kujiandikisha cha Kambangwa leo jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC), akiweka vidole vya mwanachi kwa ajili ya kuchukua alama katika zoezi la uandikishaji Daftari la Wapiga katika mfumo wa BVR katika Kituo cha Msisiri ,Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Wananchi wa Kata ya Mwananyamala wakiwa katika foleni  kujiandikisha katika Daftari la Kudumu Mpiga Kura katika mfumo wa wa alama za vidole (BVR)leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).

No comments: