Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Saada Mkuya Salum akizungumza katika siku ya pili ya mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu ufadhili wa maendeleo ( FFD3) unaoendelea jijini Addis Ababa- Ethiopia
Na Mwandishi Maalum,
New York
Mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu ufadhili wa maendeleo, ( FFD3) jana (jumanne) umeingia siku yake pili ambapo Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Saada Mkuya Salum alielezea matumaini ya Tanzania juu ya matokeo ya mkutano huo katika kusukuma mbele ajenda ya maendeleo endelevu.
Waziri wa Fedha ambaye anamwakilishi Mhe. Rais Jayaka Mrisho Kikwete katika mkutano huo, amesema kuwa, Tanzania inaamini kwamba ufadhili wa maendeleo ni moja ya ajenda muhimu kwa Bara la Afrika . Kwa sababu hiyo Tanzania, inategemea kuona ufadhili huo unakuwa na matokeo makubwa katika kuondoa umaskini katika nchi nyingi za Afrika.
“ Kama kweli tunataka kuwa na utekelezaji wa uhakika wa malengo ya maendeleo endelevu baada ya 2015, Matumaini ya nchi yangu ni kuona kuwa mkutano huu unatoka na matarajio mathubuti yatakayo hakikisha mtiririko usio shaka wa rasilimali kuchagiza maendeleo”. Amesema Mhe.Waziri
Ametoa wito wakuwapo kwa mikakati ya pamoja baina ya pande zote, kule zitokako au asili ya raslimali hizo na nchi zinazopokea misaada hiyo lengo likiwa kudhibiti mrititiko wa fedha chafu, uwezeshwaji wa kukomboa raslimali na kuzirejesha raslimali hizo kwa nchi husika.
“ Afrika inapoteza karibu dola bilioni 50 kwa mwaka kutokana na mtiririko wa fedha chafu kutoka nchi zinazoendelea, hali inayosababisha kusababisha uhaba mkubwa wa hazina ya fedha za kigeni, kupungua kwa makusanyo ya kodi, kufutwa vyanzo vya uwekezaji uwekezaji na hatimaye kuongezeka kwa umaskini”. Amesema Waziri wa Fedha.
Kiongozi huyo wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo, ameelezea umuhimu wa Mkakati wa Addis Ababa kujielekeza na kuwa mfumo madhubuti utakaoimarisha ushirikiano katika masuala ya kodi.
Vile vile Waziri wa fedha, amesisitiza kwamba takwimu zitakazotumiwa na Taasisi ambazo zitapewa jukumu la kufuatilia na kufanya marejeo kuhusu ufadhili wa maendeleo , takwimu hizo ni lazime zitoke katika taasisi za takwimu ambazo zinatambuliwa na serikali ya nchi husika.
Akabinisha kwamba matumizi ya takwimu rasmi kutoka taasisi zinazotambuliwa na serikali , kutaepusha kutumiwa kwa takwimu ambazo si rasmi na hivyo kusababisha sitofahamu na migongano kati ya Nchi wanachama na Umoja wa Mataifa.
Waziri Saada Mkuya Salumu akatoa wito wa kuongezwa raslimali fedha hususani kwa nchi zinazoendelea ili ziwe na uwezo wa kuboresha mifumo yake ya ukusanyaji wa takwimu, kuzichambua na kuzifanyia tathmini.
No comments:
Post a Comment