Thursday, July 2, 2015

Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar akabidhi vifaa mbalimbali kwa Skuli ya Rahaleo..

Wanafunzi wa Skuli ya msingi Rahaleo wakimpokea Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar alipowasili katika viwanja vya Skuli hiyo kukabidhi Vifaa viliotolewa na Mwakilishi wa Rahaleo kwa Wananchi wa jimbo hilo.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Rahaleo kuhudhuria hafla ya kukabidhi Vifaa kulia Mwakilishi wa Rahaleo na kushoto Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Rahaleo Ndg Daudi Amani Bakari
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo na wanafunzi wa skuli hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Wanafunzi wa skuli ya msingi rahaleo wakimsikiliza Mhe Waziri Zainab akitowa nasaha zake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa 

No comments: