All Right Receved by MR.PENGO 2016

Friday, July 24, 2015

DR.MARY MWANJELWA USHINDI WA KISHINDO UBUNGE VITI MAALUM MKOWA WA MBEYA KWA ASILIMIA 97 KWA MARA YA PILI BUNGENI...

Mgombea ubunge viti maalum mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa aibuka mshindi katika kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya na kupata ridhaa ya kulejea tena katika kiti  cha ubunge viti maalum mkowa wa mbeya kwa ushindi wa kishindo wa asilimia 97 na kuwashinda wagombea kumi (10) kati ya kumi na moja (11) walio kuwa wakigombea na kutaka kuteuliwa na wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya...Picha zote Na Fadhiri Atick Mbeya.
Mshindi wa ubunge viti maalum kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa akiwashukuru wajumbe wa ccm mkowa wa mbeya mara baada ya ushindi katika uchaguzi wa kumpata mbunge viti maalum mkoa wa mbeya ulio fanyika tar:24-07-2015, katika ukumbi wa nyerere Musti jijini mbeya.
Dr.mary mwanjelwa akiwa amenyanyuliwa na wanachama sambamba na wajumbe wa ccm mkowa wa mbeya kumshangiria kwa ushindi alio upata..
Furaha ikiwa imetawala katika uso wa mshindi wa ubunge viti maalum mkoa wa mbeya ndugu, Mary Mwanjelwa...
Mshindi wa ubunge viti maalum mkoa wa mbeya mh.DR.Mary Mwanjelwa akiendelea kutoa shukrani kwa wajumbe wa chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya walio mpa ridhaa ya kumchaguwa kuwa mbunge viti maalum mkowa wa mbeya..
hivi ndivyo hali ilivyo kuwa..

No comments: