Thursday, July 16, 2015

DKT MAGUFULI NA MH SULUHU WALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE ZANZIBAR LEO..

 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.

Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

 Maelfu ya watu wakiufuata msafara wa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli aliyeongozana na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan




 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akivishwa skafu na chipukizi wa CCM Zanzibar mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na chipukizi wa CCM nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na wazee maarufu wa Zanzibar
 Mhe. Magufuli akiwasili kwenye kaburi la muasisi wa Mapinduzi na Rais wa Kwanza wa Serikali Mapinduzi ya Zanzibar ,Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John P.Magufuli pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiomba dua mbele ya kaburi la Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar.


 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni kwenye Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.


 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli nje ya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwenye sherehe fupi ya kutambulishwa wagombea wa CCM kwa wanachama wa CCM.
  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Mwenza Mhe. Samia Hassan Suluhu.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Magufuli akiwasalimu wananchi waliojitokeza kwenye sherehe fupi za kumtambulisha kwenye viwanja vya Afisi Kuu CCM Zanzibar.

 Kila mtu alitaka kumgusa.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar kwenye sherehe fupi ya kumtambulisha kwa wanachama pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Ali Mohamed Shein.
 Wananchi wakishangilia



 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kushuhudia sherehe fupi za kutambulishwa kwa wagombea wa nafasi ya Urais kwa kupitia CCM kwenye viwanja vya Afisi Kuu.



 Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Mhe. Hassan Suluhu Hassan akizungumza kwenye sherehe fupi za utambulisho nje ya Afisi kuu ya CCM Zanzibar.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akiwasalimu wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye sherehe za kumtambulisha yeye na mgombea mweza kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar.
 Wakazi wa Zanzibar wakimsikiliza mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgombea wa ueais kwa kupitia CCM Dk.John Magufuli.

No comments: