Tuesday, June 2, 2015

WAKUU WA WILAYA ZA KISHAPU NA SHINYANGA WATEMBELEA MABANDA YA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA SIDO KANDA YA ZIWA.

Maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa/kutengenezwa kutoka Viwanda Vidogo  yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo SIDO kanda ya ziwa yanaendelea katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga,watu mbalimbali wanafika kujionea mambo mazuri yanayofanywa na wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.Leo jioni,Juni 01,2015 wakuu wa wilaya za Kishapu na Shinyanga wametembelea mabanda mbalimbali.Kilele cha maonesho hayo ni Juni 02,2015.

Hapa ni katika banda la Chuo cha VETA Shinyanga,wanafunzi wa chuo hicho wakionesha mtambo wa umeme wa jua na Tanesco kwa wakuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku na wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

Mwanafunzi wa VETA Asha Hamis akitoa maelezo namna ya kufanya shughuli mbalimbali kwa kutumia mitambo hii,hapa chini
Greda na Loader
Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu,Wilson Nkhambaku,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga Athanas Moshi wakiwa katika banda la watengenezaji wa bidhaa zinazotokana na mbao mfano,kabati,vitanda,sofa n.k
Wajasiriamali kutoka Kambarage mjini Shinyanga wakionesha kabati la kisasa zaidi
Hapa ni katika banda la wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za vyuma
Hapa ni katika banda la mgodi wa Almas wa Mwadui,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akipata maelezo juu ya mradi wa ufugaji nyuki na mazao yanayotokana na nyuki
Wakuu wa wilaya na wananchi wakila Popcon za wajasiriamali kutoka Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bidhaa za wajasiriamali kutoka Kenya
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiwa ameshikilia mkanda unaotokana na ngozi ya samaki.
Mjasiriamali akionesha ngozi ya samaki inayotumika kutengeneza mikanda 
Mjasiriamali akionesha bidhaa za shuleni na majumbani
Wakuu wa wilaya wakiwa katika mabanda yanayouza dawa za asili 
Hapa ni katika banda la Jeshi la zimamoto na Uokoaji mkoa wa Shinyanga,sajenti  Benjamin Kinenge akitoa maelezo namna jeshi hilo linavyofanya kazi kwa kutumia dhana mbalimbali

No comments: