Susana Koillah, Mama Shughuli na mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika semina hiyo akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) kabla ya kutafsiri mada yake kwa wanasemina.
Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Mathias Herman (kushoto) akitoa maelekezo kwa wana semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi shule za sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.
WAKUU wa jamii ya Kimasai wa Afrika Mashariki wameridhia kuachana na mila potofu zimezopitwa na wakati ikiwemo vitendo vya ukeketaji kwa wasichana wa jamii ya kimasai ambavyo vimekuwa vikiwaathiri wasichana hao kwa kiasi kikubwa.
Kauli ya kusitisha vitendo hivyo ilitolewa juzi Wilayani Ngorongoro na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na msaidizi wake kutoka Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni walipokuwa katika semina ya elimu ya afya ya uzazi, kupinga vitendo vya ukeketaji pamoja na mimba za utotoni.
Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Afrika Mashariki, Olaiboni Simeli alimueleza Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) na Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues kuwa jamii hiyo ya wamasai imeridhia kuacha mila zilizopitwa na wakati na itaendelea kushiriki kuelimisha jamii yao zaidi juu ya madhara ya mila hizo potofu ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni.
"...Tunaishukuru UNESCO kwa kuendelea kutoa elimu hii kwetu juu ya mila potofu nasisi tunaungana nanyi kuendelea kutoa elimu kwa jamii yetu kupinga ukeketaji na ndoa za utoto tumeelezwa athari nyingi zinazowapata wasichana wanaokeketwa...kwanini tuendelee na mila zinazoleta madhara kwa watu wetu? Tushirikiane kupiga vita hivi," alisema Olaiboni Simeli akizungumza mbele ya Bi. Rodrigues.
Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Naimado Olaiboni alisema hakuna haja ya jamii ya kimasai kuendelea na mila zilizopitwa na wakati ilhali mila hizo zikiendelea kuwaathiri wamasai na kuwabakiza nyuma kimaendeleo katika nyanja mbalimbali. "...Tutaendelea kushirikiana nanyi kupinga ndoa za utotoni kwa kuwa tumeelezwa madhara yake na wataalamu leo," alisema Naimado Olaiboni.
Naye Mkuu wa Shirika la UNESCO na Ofisa Mwakilishi wa Shirika hilo Tanzania, Bi. Rodrigues alisema anapenda kuona Jamii ya Kimasai inaendeleza mila na tamaduni zao lakini zile nzuri ambazo hazina chembe ya kiunyanyasaji kwa makundi yote. Alisema ukeketaji kwa wasichanga unamadhara makubwa kwa jamii hiyo hivyo haina budi mila hizo kupuuzwa ili kumlinda mtoto wa kike na madhara yanayomkumba anapofanyiwa vitendo hivyo.
"...Napenda kuona Wamasai wanaendeleza mila na tamaduni zao lakini ziwe nzuri na zisizo na chembe ya ukatili wala unyanyasaji, tuangalie ni namna gani tunaziendeleza na kubaki katika uhalisia wetu...nawahakikishia tutashirikiana kuhakikisha hili linafanikiwa kwenu," alisema Bi. Rodrigues akizungumza katika semina hiyo.
Aidha aliwashauri jamii ya Kimasai kupunguza kuwa na idadi kubwa ya watoto na wake ilhali mume akishindwa kuihudumia familia hiyo jambo ambalo limeendelea kuchochea umaskini wa familia hizo vijijini kwani watoto wamekosa mahitaji ya msingi katika familia na kujikuta wakiishi kwa taabu.
Aliwataka Wamasai pia kupinga ndoa za utotoni kwani mabinti wadogo wanapoolewa wanakosa fursa ya elimu pamoja na kuunda familia bora kutokana na uduni wao katika masuala ya afya ya uzazi kiujumla na madhara yanayowaandama katika maisha yao. "...Ndoa za utotoni nazo ni tatizo katika jamii yetu, tuzipige vita maana mtoto mdogo anapoolewa haweza kuunda familia bora na wala uzazi wake hauwezi kuwa bora...," aliongeza Bi. Rodrigues.
Zaidi ya wanasemina 210 kutoka Kata za Ololosokwani, Arash, Soit Sambu, Oloipili, Aoliani Magaidulu wakiwemo viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari na wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii Wilayani Ngorongoro wamenufaika na semina hiyo ya jitihada za kuelimisha jamii juu ya mila na desturi zilizopitwa na wakati.
Kutoka kushoto ni Mshauri na Mkufunzi wa Masuala ya Vyombo vya Habari Jamii kutoka UNESCO Tanzania, Rose Haji pamoja na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na UNESCO juzi.Baadhi ya washiriki wa semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakifuatilia mada kwenye semina hiyo.Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Emanyata Ololosokwani na Mwenyekiti warsha hiyo, Ole Daniel akitafsiri kwa lugha ya kimasai mada ya Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) alipokuwa akiwasilisha.Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kushoto) akimsikiliza Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli (kulia) kwenye semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro.Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Baadhi ya washiriki wa semina hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) wakichangia mada mbalimbali.Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Susana Koillah, Mama Shughuli na mtafsiri wa lugha ya Kimasai katika semina hiyo akisisitiza jambo. Kulia ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues.Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akiwasilisha mada katika semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro. Semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Sehemu ya washiriki wa semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni (kushoto) akichangia mada katika semina ya viongozi mbalimbali wa jamii ya kimasai, wazazi, viongozi wa shule za msingi na sekondari Wilayani Ngorongoro, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilaya ya Ngorongoro. Wengine ni wasaidizi wa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli wakishiriki semina hiyo.Baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania wakiwapongeza viongozi wa jamii ya kimasai, Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni mara baada ya semina kumalizika.Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Afrika Mashariki, Mokombo Olaiboni Simeli pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni wakipiga picha za kumbukumbu na baadhi ya maofisa kutoka Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania baada ya semina kumalizika. Kulia ni Ofisa Mradi Elimu wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Jennifer Kotta akijiandaa kuwapongeza viongozi wakuu wa jamii ya kimasai Afrika Mashariki na Tanzania walioshiriki semina hiyo.Ofisa HIV na Elimu ya Afya Taifa wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Mathias Herman (kulia) akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Sangau Naimado Olaiboni (kushoto) mara baada ya semina ya viongozi wa jamii ya kimasai, wazazi, wakuu shule za sekondari, wakuu wa idara ya afya na vitengo vya ustawi wa jamii wilayani Ngorongoro wakiwa kwenye semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro juzi.Imeandaliwa na www.thehabari.com, Ngorongoro .
No comments:
Post a Comment