Monday, June 1, 2015

TAMASHA LA KOMAA CONCERT LILIVYOFANA NDANI YA KIOTA CHA MARAHA CHA DAR LIVE JIJINI DAR.






  








 Uongozi pamoja na Wafanyakazi wa kituo cha radio ya EFM 93.7 kwa pamoja wakikata keki kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa kituo hicho ambacho kwa sasa kinakuja kwa kasi jijini Dar na kwingineko,hafla hiyo ilikwenda sambamba na kuadhimisha miaka 16 ya msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature,katika tamasha lililoitwa  KOMAA CONCERT,ambalo lilifanyika ndani ya kiota cha maraha cha Dar Live,Mbagala jijini Dar mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki na wapenzi wa muziki . 

Lengo la kuwaburudisha Mashabiki wa Juma Nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM  ilikuwa pia ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Baadhi ya Wasanii walioshiriki kulinogesha tamasha hilo ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi. Katika tamasha hilo lililowavutia wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake,kiingilio kilipangwa kuwa ni shilingi 7,000 tu. 

Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss ssebo alisema kuwa wanaamini Msanii Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya,alisema na kuongeza kuwa lakini kwa Efm huyo ni msanii wa Kwanza tu na itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwa kuwa wanaaamini Muziki unaongea. 
Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akiongoza jopo la wafanyakazi wenzake kukata keki 
Pichani kulia ni Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7 Deniss Ssebo akizungumza jambo mbele ya mwashabiki na wapenzi wa muziki na pia wasikilizaji wakubwa wa kituo hicho kuhusiana na utaratibu mzima wa sherehe hiyo,kulia ni Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akigawa keki kwa mashabiki waliofika kushuhudia tukio hilo ndani ya Dar Live. 
 Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akitumbuiza jukwaani mbele ya mashabiki wake,pia akiwashukuru kumpa sapoti ya kutosha tangu ameanza muziki na sasa anatimiza miaka 16 katika tasnia hiyo adhimu.
Wakongwe pamoja  Juma Nature na Prof.Jay wakishoo love kwa mashabiki wao.
Msanii Snura na Madansa wake wakilishambulia jukwaa la KOMAA CONCERT
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Shetta akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la KOMAA CONCERT.
 Makamuzi yalikuwa yakiendelea jukwaani. 
 amsha amsha za hapa na pale zikiendelea jukwaani.
 Mashabiki walikuwa kibao. 
 Deejay Spar akionesha uwezo wake kwa mashabiki. 
 Shabiki wa ukweli kwa Juma Nature
 Burudani ilipangwa sawa bin sawia huku Ma -Mc wakinogesha shughuli
  Mashabiki na mandhari ya Dar Live kwa usiku huo ndani ya jicho la samaki
 Dar Live palinoga usiku huo wa KOMAA CONCERT 


 Mtangazaji mahiri wa EFM Capt.Gadn G Habash akizungumza jambo mbele ya mshabiki
  Kila alieweza kuchukua kumbukumbu kwa aina yake,ilikuwa ruksaa.
Dj Majay akihakikisha mambo yanakwenda sawa

No comments: