Sunday, June 7, 2015

SERIKALI:TUENDELEE KUSHIRIKIANA NA WADAU WA VIJANA.

Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Gofrey Nyaisa akizungunza na vijana wa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzio wa Programu ya Kukuza ajira zenye Staha kwa vijana wa mkoa huo (YEID) juzi jijini hapa.Program hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano wa asasi za kirai za Open Mind Tanzania (OMT), Tanzania Youth Vision Association (TYVA) na Youth for Africa (YOA).
Mratibu wa Programu ya kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam, kupitia Elimu ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Dominic Ndunguru akizungumza na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Programu hiyo juzi jijini Dar es Salaam. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
Baadhi ya Vijana waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam wakiangalia baadhi ya huduma zitolewazoi na asasi mbalimbali za Vijana walipofanya maonyesho yaliyoenda sambamba na uzinduzi huo juzi katika viwanja vya Don Bosco Youth Center jijini Dar es Salaam.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Gofrey Nyaisa akikabidhi Cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Maendeleo ya Biashara na Ujasiriamali Bi. Lilian Daniel wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza ajira zenye Staha kwa vijana wa mkoa wa Dar es Salaam (YEID) juzi jijini hapa. Jumla ya vijana 105 kutoka katika masnispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni walipata mafunzo hayo yanayoendeshwa na asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kundi la Youth Can wakiimba wimbo wao ujulikanao kwa jina la “Tuyalinde” unaohamasisha utunzaji wa mazingira wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha kwa Vijana (YEID) juzi jijini Dar es Salaam. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT) na Youth For Africa (YOA).

Baadhi ya washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha kwa Vijana wa mkoa wa Dar es Salaam (YEID) wakifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa na vikundi mbalimbali juzi jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha kwa Vijana wa mkoa wa Dar es Salaam (YEID) amabaye pia ni Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa (wapili kulia) akiwa katika picha yenye bango linalohamasisha vijana kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura juzi jijini Dar es Salaam.
Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gofrey Nyaisa (wa tano kutoka kuliawaliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Vijana walio tunukiwa vyeti baada ya kuhitimu mafunzo ya Maendeleo ya Biashara na Ujasiriamali wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza ajira zenye Staha kwa vijana wa mkoa huo (YEID) juzi jijini hapa.Program hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano wa asasi za kirai za Open Mind Tanzania (OMT), Tanzania Youth Vision Association (TYVA) na Youth for Africa (YOA). Picha Zote na Frank Shija, WHVUM 

Na: Frank Shija, WHVUM
Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote walio na dhamira na mueleko wa dhati katika kuhakikisha tunatatua changamoto za ajira kwa Vijana nchini.
Kauli hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa alipokuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha kwa Vijana wa mkoa wa Dar es Salaam (YEID).
Nyaisa amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukulia kwa uzito stahiki suala la ajira kwa vijana ikiwemo kuanzisha program mbalimbali kwa lengo la kumsaidia kijana aweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na changamoto za ajira zinamzomkabili kijana.
Aliongeza kuwa mpaka sasa Serikali imekwisha tekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuwapa mafunzo vijana ambapo jumla ya vijana 1550 wamekwisha pati wa mafunzo ya ujasiriamali na stadi za maisha kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana na kusongeza kuwa mafunzo hayo ni endelevu.
“Niseme tu Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wenye dhamira ya dhati ya kumletea maendeleo kijana ili aweze kujikwamu” Alisema Nyaisa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mratibu mwenza wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha kwa Vijana wa mkoa wa Dar es Salaam (YEID) kupitia Elimu ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Dominic Ndunguru amesema kuwa imekuwa ni faraja kwao kupata ushirikiano kama huo kutoka Serikali hii na kuongeza kuwa hii ni dalili njema kwao kuwa Programu hiyo itakuwa na matokeo chanya na kwa muda mfupi.
Ndunguru alisema kuwa Programu hiyo ya Kukuza Ajira zenye Staha ilianza kama majaribio tokea mwaka 2014 na kuonyesha mafanikio hivyo ni furaha kwao kuone leo (juzi) inazinduliwa rasmi ikiwa tayari imeleta matunda kwa vijana.
Aliongeza kuwa kupitia Programu hiyo vijana watapata fursa ya kupata bure elimu ya Ujasiriamali na Maendeleo ya Biashara, taarifa mbalimbali zinzaohusu vijana, na fursa ya kushiriki mafunzo ya stadi za maisha na matumizi ya Tehama.
Kwa upande wake mmoja wa Vijana walionufaika na Programu hiyo Bi. Lilian Daniel kutoka Manispaa ya Temeke ameelezea kufurahishwa kwake na ujio wa Programu hii kwa kuwa imemfanya apate ujasiri wa kuthubutu kufanya maamuzi katika masuala mbalimbali.
Ameongeza kuwa Programu hiyo itasaidia sana kwa kuwa inatoa fursa ya kupata elimu ya bure hivyo kwa wasiokuwa na uwezo wa kuendelea na elimu ya Sekondari na ata vyuo wanayo fursa ya kuelimika kupitia Progra hii iliyozinduliwa rasmi leo. Alisema Lilian

Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha kwa mkoa wa Dar es Salaam ambayo kwa kiingeraza inaitwa Youth Employability Initiative in Dar es Salaam (YEID) inatekelezwa kwa ubia baina ya asasi tatu za kirai ambazo ni Tanzania Youth Vision Association (TYVA), Open Mind Tanzania na Youth for Africa (YOA) katika Manispa za Ilala, Temeke na Kindoni jijini Dar es Salaam.

No comments: