Wednesday, June 10, 2015

NUSU FAINALI YA MTEMVU CUP YAPIGWA MWEMBE YANGA.


 Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwa sambamba na Mbunge Jimbo la Temeke, Mh. Abbas Mtemvu (kati) kwenye viwanja vya Mwembe Yanga wakifuatilia mpambano kati ya timu ya Mtoni dhidi ya Kata ya 14, zilipokuwa zikichuana ambapo katika mchezo huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3.
  Viongozi mbalimbali wa Michezo   wajitokeza katika viwanja vya Mwembe Yanga wakifuatilia mpambano kati ya timu ya Mtoni dhidi ya Kata ya 14, zilipokuwa zikichuana ambapo katika mchezo huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3. kuanzia kulia  walio kaa ni mweka hazina timu ya Sandali,  wakatkati ni Katibu wa Timu ya Kata ya Miburani , ambayo timu yake ya inacheza leo na timu ya  Kilakala na Meneja na Mwenyekiti wa Michezo Mwembe Yanga Dar es Salaam
 Promoter Bonge na Mkurugenzi wa Timu ya 14,   akizungumza na wachezaji walipokuwa wamepumzika kipindi cha mapumziko  katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam

 Wachezaji wa Timu ya Kata ya 14 wakishangilia kwa pamoja wakiwa na kipa wao baada ya kushinda kwa mikwaju ya Penalt katika Nusu Fainal ya Mtemvu Cup   Kati ya timu ya kata ya  14 na Mtoni
 Msanii Omar Tego Coast Modern Taarab akitoa burudani wakati wa Nusu Fainali ya Mtemvu Cup lipokuwa ikiendelea Viwanja vya  Mwembe Yanga
 Msanii Inspekta Harun , Haruna Kahena akiwa mmoja wa wasanii hao waliotoa burudani wakati wa Nusu Fainal ya Mtemvu Cup katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam

 Mshambuliaji wa timu ya Mtoni, Samwel Salonge  (kulia) akimtoka beki wa timu ya timu ya Kata ya 14,katika mpambano wa Nusu Fainal  ya  Mtemvu Cup  kwenye Uwanja wa Mwembeyanga  Dar es Salaam jana,  Mtanange  huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3


  Mshambuliaji wa timu ya Mtoni, Rajabu Zanda akimtoka beki wa timu ya timu ya Kata  14,katika mpambano wa Nusu Fainal  ya  Mtemvu Cup  kwenye Uwanja wa Mwembeyanga  Dar es Salaam jana,  Mtanange  huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3
 Mashabiki wakifatilia mpambano huo.(PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)

No comments: