All Right Receved by MR.PENGO 2016

Sunday, June 7, 2015

NAIBU WAZIRI WA MAILIASILI NA UTALII AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA KILIFAIR 2015.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Moshi Club kwa ajili ya kufungua rasmi maonesho ya kimatifa ya Kitalii yajulikanayo kama KiliFair 2015.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akisalimiana na Naibu waziri wa Habari Utamaduni,Utalii na Michezo wa Zanzabar Bi Hindi Khamis walipokutana katika maonesho hayo.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo,Naibu waziri wa utalii,Mohamed Mgimwa akiwa katika picha ya pamoja na iongozi wengine akiwemo kaimu mkuu wamkoa wa Kilimanjaro,Dkt Charles Mlingwa,katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa,Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Rufunguro.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akiwa ameambata na naibu waziri wa habari,utamaduni ,utalii na Michezo Zanzibar,Bi Hindi Khamis alipokuwa akitembelea banda la maoensho ya utalii la Zanzibar.
Naibu Waziri ,Mgimwa akizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya utalii ya Zara tour 
Naibu Waziri ,Mgimwa akinywa kahawa alipotembelea banda la kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines.
Waoneshaji wengine walibuni mbinu zaidi wakiwatumia wafugaji jamii ya maasai katika maonesho hayo.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro KINAPA,Erastus Rufunguro akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Asante Tour ,Cuthbert pamoja na mkurugenzi wa Kilifair ,Tom.
Naibu waziri Mgimwa akizungumza na Cuthbert.
Naibu Waziri wa maliasili na utalii akisalimiana na Meneja Biashara wa kampuni ya Kibo Palace ,Charity Githinji ,wakati Naibu waziri alipotembelea banda hilo.
Baadhiya wafanyakazi wa kampuni ya Kibo Palace wakiwa katika banda lao la maonesho 
Naibu waziri wa utalii Zanzibar Bi Hindi akipokea zawadi toka Kibo Palace.
Manaibu waziri wa utalii,Tanzania bara na Zanzibar,Mgimwa na Bi Hindi wakiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa Kilifair Dominic Shoo na Tom.
Mkurugenzi wa kampuni ya Kilifair ambao ndio waandaji wamaonesho hayo ,Dominic Shoo akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo .
Naibu waziri wa habari,utamaduni,utalii na Michezo Zanzibar ,Bi Hindi Khamis akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
Baadhi ya wageni waliofika kwa ajili ya maonesho hayo.
Naibu Waziri ,Mgimwa akitoa hotuba yake ya ufunguziwa maonesho ya kimataifa ya utalii ya Kilifair 2015 yanayofanyika katika viwanja vya Moshi Club.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu waziri Mgimwa akiteta jambo nammoja wa wakurugenzi wa kampunu ya Kilifair Dominic Shoo.
Kikundi cha burudani toka nchini Kenya kikitoa burudani katika maonesho hayo.
Baadhi ya mabanda yaliyopo ndani ya viwanja vya Moshi Club yakionesha bidhaa na huduma zitolewazo na kampuni mbalimbali za utalii.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Post a Comment