Saturday, June 20, 2015

MH. LOWASSA APATA UDHAMINI WA WANACCM 69,462 KATIKA MIKOA YA IRINGA NA NJOMBE...

 Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Iringa, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Samora Mkoani humo, kumpokea Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja huo tayari kwa kukabidhiwa fomu za WanaCCM waliomdhamini ili  kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Iringa wamevunja rekodi ya Mbeya kwa uwingi wa wanachama waliomdhamini Mh. Lowassa, amepata wadhamini 58,562 kwa mkoa wa Iringa pekee na ukiongeza na wanaCCM 10,900 wa mkoa wa Njombe alikopita pia kupata udhamini, unafanya jumla kuu ya wadhamini wote kufikia 69,462. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Samora Mkoani Iringa, tayari kwa kukabidhiwa fomu za WanaCCM waliomdhamini ili  kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Iringa waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Samora Mkoani humo.
Umati wa Watu wa Iringa.
Ujumbe kutoka kwa Rafiki wa Lowassa.
Sehemu ya WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdenburg Mdegela akisoma Neno kutoka kwenye simu yake.


Sehemu ya WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakionekana ni wenye furaka kubwa baada ya kusikia Neno kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdenburg Mdegela.
Chifu wa Wahehe wa Mkoani Iringa, Chifu Hassan Adam Sapi  akizungumza machache na kutoa baraka za kichifu kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa katika Safari yake ya Matumaini.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipena mikono na Chifu wa Wahehe wa Mkoani Iringa, Chifu Hassan Adam Sapi mara baada ya kupewa baraka hizo.
Salaam na Machifu wa Mkoa wa Iringa.
Bibi huyu alijikuta akibubujikwa na machozi baada ya maneno ya Chifu wa Wahehe wa Mkoani Iringa, Chifu Hassan Adam Sapi kumuingia.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa mjini akikabidhi fomu za WanaCCM waliomdhamini Mh. Lowassa ili kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakati akitoa shukrani kwa waliomdhamini ili kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. amepata wadhamini 58,562 kwa mkoa wa Iringa pekee.
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku akiimba moja ya nyimbo zake wakati akiwasalimia wanaIringa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana baadhi ya Wazee wa Mkoa wa Iringa.
Mh. Lowassa akiwaaga wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Iringa.
Akiwa safarini kutokea Mkoani Mbeya kuelekea Mkoa wa Njombe, Mh. Lowassa akilimamishwa na WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mji wa Igurusi Wilayani Mbarali mkoani Mbeya ili azungumze nao kidogo.
Vijana wa Bobadoba wa Mkoa wa Njombe walijitokeza kwa wingi wao kumpokea Mh. Lowassa wakati alipowasili mkoani hapo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mh. Luhingo Rweyimamu.
Akizungumza na mmoja wa Watoto wa Mji wa Njombe alikuja kumsalimia.
Akiwapungia WanaCCM na Wananchi wa Mji Njombe.

Dkt. Chegeni akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Njombe waliokuwa wamekusanyika kwa wingi kwenye Uwanja wa CCM wa Turbo.






Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu 10 wa Mkoa wa Njombe waliomdhamini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Njombe, Clemence Mponzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Njombe wakati akitoa shukrani kwa waliomdhamini ili kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mkoa wa Njombe alipata Udhamini wa WanaCCM zaidi ya elfu 10.

Makambako.
Mh. Lowassa akisalimiana na WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mji wa Makambako Mkoani Njombe waliomsimamisha wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Iringa.
Akiangalia Burudani ya Ngoma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Marafiki zake ambao ni Wakazi wa Mji wa Makambako, Alfred Mtweve (kulia) na Angelusi Muhingu wakati aliposimama kuwasalimia WanaCCM na Wananchi wa Mji huo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akifurahi jambo na Marafiki zake.
Mh. Lowassa akiwashukuru WanaCCM na Wananchi wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe waliomdhamini.
Kwaherini WanaMakambako.
"Kidumu Chama cha Mapinduzi"
Mh. Lowassa akivishwa skafu na Kijana wa Chipukizi wa CCM Wilaya ya Mufindi.
Mh. Lowassa, akifurahi jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoani Iringa, Jesca Msambatavangu (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita

Mkuu wa wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita akiwasalimia WanaMufindi.
Shangwe tupu kwa WanaMufindi.



No comments: