Tuesday, June 16, 2015

MASHINDANO YA MTEMVU CUP YAFIKIA TAMATI, KATA YA 14 YAIBUKA KIDEDEA.

Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akiwa na Waziri wa Habari  Vijana Utamaduni na Michezo, Dk.Fenellah Mukangala (kulia), wakati akizungumza na wananchi baada ya kumalizi kwa fainali hizo.

Nahodha wa Timu ya Kata 14,Uhuru Selemani akiwa ameinua kombe baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Waziri wa Habari  Vijana Utamaduni na Michezo, Dk.Fenellah Mukangala baada ya kuibuka washindi.
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (kushoto), akiwa na Waziri wa Habari  Vijana Utamaduni na Michezo, Dk.Fenellah Mukangala (kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali za mashindano ya Mtemvu CUP yaliyofikia tamati viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana. Timu zilizoingia ingia fainali hiyo ni Miburani Kata ya 15 na Kata ya 14 ambayo iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao 1-0.
Mashabiki wakiwa kwenye fainali hizo.




Mchuano ukiendelea.
Hapa ni kazi tu kwa kwenda mbele.


Vikombe na mipira vilivyotolewa kwa washindi.

Waratibu wa mashindano hayo yaliyohusisha kata zote za wilaya hiyo wakiwa kwenye fainali hizo.

Na Mwandishi wetu

BAADHI ya wadau wa mpira wa miguu nchini wameiomba serikali kumpa ushirikiano  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu kufuatia kuanzisha michuano ya soka kwakuwa anatambua umuhimu wa vijana kuendelezwa.

Hayo yalisemwa jana na wadau hao mada baada ya mchezo wa fainali ya ya kombe la Mbunge wa Temeke, Mtemvu Cup ikiwa ni muda mfupi baada ya    Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Dk. Fenellah Mukangala   alipokuwa akikabidhi zawadi za washindi wa kombe hilo la Mbunge wa jimbo la Temeke  ambapo timu ya Temeke Kata ya 14 ilifanikiwa kuibuka mshindi wa kombe hilo na kupatiwa kikombe na pesa tasilimu sh. mil 1.5 huku Miburani Kata 15 wakiambuliwa sh mil 1 na kikombe kama washindi wa pili na nafasi ya tatu ilichukuliwa na timu ya Kilakala ambayo ilipatiwa sh 750,000 na kikombe kama mshindi wa tatu.
Mukangala aliwaomba madiwani wa Manispaa ya Temeke kufanya jitihada za kuujenga Uwanja wa Mwembe Yanga kuwa wakisasa zaidi ili utumike kwa ajili ya kupata vipaji vya michezo vya vijana wa manispaa hiyo pia kuwaingizia kipato kutokana na viingilio.
Wakizungumza Dar es salaam jana wadau  huyo alisema kuwa Mtemvu ni  kiongozi anayeendeleza michezo nchini hivyo vijana watumie fursa hiyo.
Walisema kuwa michezo ni moja ya sera ya kutoa ajira kwa vijana ambao wameamua kujiajiri kupitia michezo hivyo kuna haja ya vijana kutambua jitihada hizo.
Hata hivyo wadau hao wamekiri kuwa serikali ya awamu ya nne ndiyo serikali iliyochangia kukuza michezo nchini.
Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu ameahidi kuendelea kuwekeza nguvu zake zote katika michezo ili kupata vipaji ambayo vitaitangaza nchini kimataifa.
"N ahidi kuendelea kukuza vipaji vya vijana,kwakuamua kuendeleza na kukuza soka ili tanzania iwe kujulikana zaidi nje na "alisema.
Alisema ataendeleza mashindano hayo hata kama hatachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

No comments: