Sunday, June 14, 2015

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AMUAGA BALOZI WA BRAZIL ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango wakimsikiliza kwa furaha Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe.Francisco Suarez Luz (kushoto) kabla ya kuanza kwa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa ajili ya kumuaga Balozi Luz. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 13 Juni, 2015.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula kwa pamoja na Balozi Mpango wakiendelea kumsikiliza Balozi Luz mara baada ya kuketi tayari kwa kushiriki chakula cha mchana kwa heshima ya kumuaga Balozi Luz.
Meza Kuu wakiwemo Mabalozi kutoka nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Brazil aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Francisco Suarez Luz. Katika hotuba yake alimshukuru Balozi huyo kwa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili katika kipindi chote alichokuwepo nchini na kumuomba aendelee kuwa Balozi mzuri kwa kuitangaza Tanzania.
Balozi Luz pamoja na Mablozi wengine wakimsikiliza Balozi Mulamula ambaye haonekani pichani
Balozi Luz nae akitoa hotuba yake ambapo aliisifu Tanzania kuwa ni nchi ya amani na kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula pamoja na Mabalozi wengine wakimsikiliza Balozi Luz (hayupo pichani)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula na Balozi Luz wakigonga glasi kama ishara ya kuutakia heri ushirikiano kati ya Tanzania na Brazil 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mulamula akimkabidhi Balozi Luz zawadi ya picha ya mchoro unaoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania. Anayeshuhudia ni Bi. Felister Rugambwa, Afisa Mambo ya Nje.
Sehemu ya Mabalozi wakishuhudia Balozi Luz akipewa zawadi (hayupo pichani)
Maafisa Mambo ya Nje nao wakifuatilia matukio wakati wa hafla ya kumuaga aliyekuwa  Balozi wa Brazil hapa nchini. Kushoto ni Bw. Leonce Bilauri na Bi. Felister Rugambwa
Balozi wa Namibia hapa nchini akiwa pamoja na Balozi wa Cuba nchini.
Balozi wa Urusi hapa nchini Mhe. Yuri Fedorovich Popov (kushoto) akimweleza jambo mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Brazil
Sehemu nyingine ya Wageni waalikwa

No comments: