Wednesday, June 10, 2015

KAMPUNI YA MIDEA YA CHINA YAINGIZA NCHINI VIYOYOZI VYA KISASA VINAVYOTUNZA MAZINGIRA VITAUZWA KWA BEI NAFUU.

Mkurugenzi Mkuu wa Changchun International Co.Ltd, Kelvin Zhao, akizungumza katika uzinduzi huo.
  Mwakilishi wa Masuala ya na Biashara wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vifaa mbalimbali na viyoyozi (AC), vinavyosambazwa na Kampuni ya Midea ya china uliofanyika Hoteli ya Hyatt Recency Dar es Salaam The Kilimanjaro leo asubuhi.
 Mwakilishi wa Masuala ya na Biashara wa China nchini Tanzania, Lin Zhiyong (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wenzake. Kutoka kulia ni Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen, Meneja wa Afrika wa Midea RAC na Vifaa vya Nyumbani, Mkurugenzi Mkuu wa Changchun International Co.Ltd, Kelvin Zhao na Meneja Masoko, Peck Zhao.
 Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Mshereheshaji wa uzinduzi huo akiongoza hafla hiyo.
  Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen (kulia), akiteta jambo na  Meneja Masoko, Peck Zhao.
 Warembo waliokuwa wakitoa huduma ya kupokea wageni 
katika uzinduzi huo. Kulia ni Rebecca Paulah na Jacky Laswai. 
 Raia wa China wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Raia wa China wakiwa kwenye uzinduzi huo
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Changchun International Co.Ltd, Kelvin Zhao, akizungumza na wanahabari.
Mratibu wa uzinduzi huo, Anna Irengo (kulia), akizungumza na wanahabari.
Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI Midea ya China inayotengeneza viyoyozi (AC) imetoa ajira kwa watanzania wapatoa 30 tangu ianze kufanya shughuli zake nchini.

Hayo yalibainishwa na  Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen, wakati akizungumza na waandishi wa habari na wadau wengine wakati wa hafla fupi ya kuzindua viyoyozi hivyo iliyofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.

Alisema ili kuingia katika soko la ushindani kampuni hiyo imejidhatiti kutoa huduma bora hasa katika kipindi hiki ambacho dunia ipo katika ukuaji wa teknolojia na uharibifu wa mazingira ambapo viyoyozi hivyo wanavyovisambaza vinasaidia kutunza mazingira.

“Mbali na kukua kwa teknolojia, vile vile tumeamua kuwekeza Tanzania ili kutoa ajira kwa watanzania na kuwanusuru na uharibifu wa mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema.

Chen alisema, viyoyozi hivyo vitauzwa kwa bei nafuu ili kumpa fursa kila mtu kuweza kununua na ni kwa matumizi ya ofisini na nyumbani.

“Viyoyozi ambavyo ni kwa matumizi ya nyumbani havitumii umeme mwingi, hivyo ni matumaini yetu tutawezesha wananchi wengi kuvitumia,” alisema.

Alisema viyoyozi vya ofisini vipo vya ukubwa mbalimbali ambapo vingine ni kwa ajili ya matumizi ya kwenye majengo makubwa.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Changchun International Co.Ltd, Kelvin Zhao, aliwataka watanzania kuzingatia kuwa viyoyozi hivyo ni vya ubora wa hali ya juu licha ya kuwepo kwa dhana potofu ya uduni wa bidhaa kutoka nchini  China.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wadau wengine kununua viyoyozi hivyo kwani ni rafiki wa mazingira.

No comments: