All Right Receved by MR.PENGO 2016

Saturday, May 16, 2015

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA KITUO CHA MAWASILIANO YA DHARURA CHA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)  Ernest Mangu, mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi, iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. Katikati (mwenye tai) ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa ambaye pia alihudhuria hafla hiyo.kULIA NI Kamishna wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Suleiman Kova.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu, katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam. Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini(IGP),  Ernest Mangu, akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe, mara baada ya kufungua kituo  cha Mawasiliano ya Dharula cha Polisi iliyofanyika katika viwanja vya kituo cha kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.Waziri Chikawe alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (wa nne kutoka kulia mstari wa kwanza), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kulia – mstari wa mbele), viongozi mbalimbali wa jeshi la Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu( watano kutoka kulia) na Wawakilishi mbalimbali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), mara baada ya uzinduzi wa Kituo cha Mawasiliano ya Dharura cha Polisi uliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Kati cha Polisi,jijini Dar es salaam.
Post a Comment