Wednesday, May 13, 2015

VIJANA WAMETAKIWA KUKOPA NA KURUDISHA MAREJESHO KWA WAKATI.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh.Norman Sigala King Alie simama. 

Vijana nchini wametakiwa kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mh. Noman Sigala King wakati wa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

Mh. King alisema Serikali imeamua kutoa mafunzo kwa vikundi vya vijana ya jinsi ya kuandaa maandiko ya miradi mbalimbali, uongozi bora na stadi za maisha ili kuwatoa katika mitazamo hasi kwenda mitazamo chanya kwa kutumia fursa zilizopo.

Amesema vijana wengi wanafursa mbalimbali za kujikwamua na umaskini lakini hawatumii fursa hizo vizuri na kubakia wakikaa vijiweni bila kujishughulisha na kazi yeyote na kuishia kuvuta madawa ya kulevya na kuwa wezi.

Nea Diwani wa kata ya Matimila jimbo la Peramiho Mh. Menesi Komba amesema mafunzo ya kujengewa uwezo ni fursa kwa vijana wa Halmashauri ya Songea kwani watakuwa wamepewa uelewa mkubwa wa jinsi ya kuendesha shughuli zao za ujasiriamali kwa ufanisi na utaalamu.

Aliwaasa vijana kutekeleza elimu hiyo kwa vitendo kwa kuwafundisha vijana wenzao ambao hawakupata bahati ya kuhudhuria katika mafunzo hayo na kuachana na tabia ya kuwa wabinafsi wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi vingine.

Nae Diwani wa kata ya Peramiho na Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii Mh. Isack Mwimba amesema elimu ya ujasiriamali, Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ikiwa ni pamoja na Stadi za maisha vitawawezesha vijana wa Halmashauri ya Songea kuwa wazalendo katika kuitumikia nchi yao na kujiinua kiuchumi.

”Jamani vijana wenzangu ifikie muda wa kujiuliza tutaifanyia nini nchi yetu badala ya kubakia na mawazo ya nini serikali yetu itatupatia”. Alisema Mh. Mwimba
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh.Norman Sigala King aliyesimama akiongea na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana (hawapo pichani) ya kujikomboa kiuchumi yanayotolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,wa kwanza kutoka kushoto ni KaimuMkurugenzi.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyesimama akitoa mada ya ujasiriamali kwa Vijana wa Halmashauri Songea wakati Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara ya mafunzoa ya kujikomboa kiuchumiMkoani Ruvuma.

Kaimu Mkurugezi wa Halmashauri ya Songea Bi. Wenisaria Swai wa kwanza kulia akiongea na ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakati wa ziara ya ujumbe huo uliopo mkoani Ruvuma kwa lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali,Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha na uongozi kwa Vijana wa Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria kutoka Wizarani Bi. Ester Riwa.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh.Norman Sigala King akisalimiana na baadhi ya vijana wa Halmashauri ya Songea wakati wa mafunzo ya kujikomboa kiuchumi yanayotolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Bw. Rajab Mtiula wa nne kutoka kushoto waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Halmashauri ya Songea wakati mafunzo ya ujasiriamali na jinsi ya kujikomboa kiuchumi yanayotolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.(picha zote na Benjamin Sawe)

No comments: