Friday, May 15, 2015

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA EPZA.

Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Mkurugenzi wa Mipango wa EPZA, Bw. Lamau Mpolo (Katikati) akizungumza na Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) wakati Bibi Mwanri na ugeni wake walipotembelea Ofisi za Mamlaka kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Mamlaka, Mabibo jijini Dar es Salaam. Anayewasikilizia ni Meneja wa Utekelezaji na Maendeleo wa Mamlaka, Mhandisi Keneth Haule (Kulia).
Bibi Lilian Kalengo (Kulia), muwakilishi wa Kiwanda cha Tooku Garments akiwaonesha suruali ya jeans wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho ni moja ya viwanda 12 vilivyoanza uzalishaji katika Ukanda wa huo.
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiangalia moja ya suruali zinazotengezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa mabinti wa Kitanzania walioajiriwa na Tooku Garments akiwa kazini.
Wakina dada wakiendelea na kazi ya utengenezaji wa suruali za jeans zinazotengenezwa na kiwanda cha Tooku Garments kilichopo katika eneo la Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA), Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mandhari ya kuvutia ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) yaliyopo Mabibo, jijini Dar es Salaam. PICHA NA SAIDI MKABAKULI

No comments: