Sunday, May 24, 2015

NYALANDU AKAGUA MADHARA YA MAMBA MLA WATU MASASI.


 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsikiliza diwani wa Nhavila, wilayani Masasi, Meja Ramadhan Chilumba, jana, katika sehemu ya mto, wakati waziri huyo alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na
mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

 Katibu Tawala wilaya ya Masasi, Dunford Peter akimwonyesha ramani Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ya sehemu ya mto huo, wakati waziri huyo alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

 Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimsaidia Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupanda kingo za mto, alipotembelea mto Ruvuma mpakani na Msumbiji kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.

 Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimwongoza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli wilayani Masasi, mpakani na Msumbiji alikokwenda kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.

 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

 Wanakijiji wa Manyuli, wilayani Masasi wakimsikiliza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumza nao jana, alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na
mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikabidhi hundi ya fidia kwa Katibu Tawala wilaya ya Masasi Dunford Peter ili zigawiwe kwa watu walioathiriwa na mamba katika vijiji vilivyo kando ya mto Ruvuma jana, ikiwa ni mpango wa serikali kufidia watu waliojeruhiwa ama kuuawa na mamba nchini.

No comments: