Sunday, May 10, 2015

DUNIA KUJADILI CHANGAMOTO NA ATHARI YA MADAWA YA KULEVYA.

Bw. Sam Kutessa, Rais  wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Na  Mwandishi Maalum, 
New York 
Jumuiya ya Kimataifa  inajiaanda  kwa  mkutano maalum na  wa aina yake kufanyika, ambapo  nchi wanachama watakutana  na  kujadiliana kwa kina kuhusu  changamoto na adhari kubwa  zitokanazo na  biashara haramu na matumizi ya dawa za kulevya.
 Mapema wiki iliyopita,    wajumbe wanaoziwakilisha nchi  zao  hapa  Umoja wa Mataifa, walikuwa na mkutano wa siku moja ambao ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano huo maalum utakaofanyika mwezi Aprili  2016.
Mkutano huo wa maandalizi uliofanyika hapa  Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo mawaziri kadhaa kutoka nchi hasa  za  Amerika ya Kati ambako   nchi nyingi zinakabiliwa  na changamoto kubwa ya  biashara hiyo, uliandaliwa na Bw. Sam Kutessa, Rais  wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika  majadiliano ya  mkutano huo ,  ilidhihirika wazi kwamba hakuna nchi hata moja   duniani  iwe tajiri au maskini ambayo  haijakumbwa  na  janga  la biashara na  matumizi ya dawa za kulevya.SOMA ZAIDI HAPA.

No comments: