Tuesday, May 5, 2015

DKT. SHEIN AFANYA ZIARA MAENEO YALIYOKUMBWA NA MAAFA YA MVUA, ZANZIBAR.


Hapa ni Mtaa wa Mwanakwerekwe ambapo pamefanyika shimo kubwa akama linavyoonekanwa kutokana na mvua iliyonyesha juzi na kupelekea uharifu ambao fedha nyingi zitatumika kufukia eneo hili pia Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea wakati alipofanya ziara ya makusudi leo kutembelea maafa mbali mbali yaliyotokea kutokana na Mvua hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Injinia Ramadhan China wa Idara ya Ujenzi wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed leo wakati wakati alipofanya ziara ya hafla ya kutembelea Maeneo ya Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia maafa mbali mbali yaliyowakumba wananchi wa sehemu hiyo kwa kuvunjikiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali (kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed (kulia) wakati wakati alipofanya ziara ya hafla ya leo kutembelea Bwawa la Maji la Mwanakwerekwe Mjini Unguja kuangalia namana lilivyofurika Maji ya mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali kwa Wananchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohamed Iddi (kulia) alipofika leo kuangalia maafa yaliyomkuta Bibi Mwanahamis Takrima Mohammed (aliyekaa) kwa kuvunjikiwa na nyumba yake kutokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi na kupelekea hasara mabali mbali (wa pili kulia) Mkuu wa Wilaya Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud.
Baadhi ya Nyumba za wananchi wa Ziwamaboga Wilaya ya Magharibi zilizoathirika kwa kuingiliwa na maji ya mvua mkubwa iliyonyesha juzi na kepelekea hasara mbali mbali kwa Wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa ziwa hilo ambapo leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alitembelea na kuona hasara zilizotokea akiwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud wakati alipotembelea baadhi ya Nyumba za wananchi wa Ziwamaboga Wilaya ya Magharibi zilizoathirika kwa kuingia na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kepelekea hasara mbali mbali, katika ziara hiyo Mhe, Rais alifuatana na Viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimfariji Bibi Fatma Abdalla Turufino Mkaazi wa Uwanja wa Farasi na Kwahani Mjini Zanzibar wakati alipofanya ziara ya hafla leo kutembelea wananchi wa sehemu hiyo waliopatwa na maafa ya kuingiliwa na maji ya mvua iliyonyesha juzi na kupelekea maafa yaliyosababisha kukosa makaazi bora.(Picha na Ikulu.)

No comments: