Friday, April 10, 2015

TASWIRA MBALIMBALI KATIKA MGOMO WA MADEREVA WA VYOMBO VYA USAFIRI LEO.

Madereva wa Vyombo vya Usafirishaji katika maeneo mbalimbali hapa nchini, leo wameingia katika Mgomo wa kutotoa huduma hiyo, kwa kile kinachoelezwa Madereva hao kutakiwa kurudi vyuoni kwa mafunzo zaidi ya usalama barabarani.

Hali ya mgomo huo, umepelekea adha kubwa kwa abiria wa vyombo hivyo, hasa wale waliokuwa wakielekea mikoani, kwani katika Stendi kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es salaam, hakuna basi hata moja lililoondoka huku daladala nazo zikiwa hazionekani kabisa vituoni.

Uongozi wa Madereva hao umeomba kukutana na Uongozi wa Juu Serikalini ili kulizungumzia swala hilo la kuwataka Madereva hao kurudi mafunzoni, kwani wao wanadai kuwa kazi wazifanyazo si za kudumu na hivyo watakaporudi mafunzoni hali ya maisha yao itatetereka.

Daladala za leo zilikuwa ni hizi, hapo ukiwa na buku mkononi unafika safari yako.


Kituo cha Daladala cha SIMU2000 a.k.a Kituo kipya cha Sinza jijini Dar.
Abiria ndani ya Pikapu...
Bodaboda ndio habari ya mujini leo.
Huku Ubungo mambo yako namna hii, ni mwendo wa kupiga mguu tu.
Mijadala ikiendelea kwa wadau mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika kituo kikubwa cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar.
Mara lori likazuiliwa na watu hawa, wakidai kuwa amepakia abiria hivyo anatakuwa kuwashusha kama anataka kuendelea na safari yake.
Walipoona Polisi wanakuja wakaliashia lile Lori na kila mmoja kukimbia eneo hilo.
Huyu akajikuta akining'inia baada ya kupigwa tanganyika jeki na Askari kanzu.
Haya ingia humooo....
Ubungo mambo yalikuwa si shwari leo.
Wengi wametembea kwa miguu leo kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.
kuna walio Shea kwa kukaa namna hii.
Ubungo Temino.
Wazee wa Feva leo wameweka kambi Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo ili kuhakikisha usalama unapatika muda wote katika eneo hilo.
Mabasi ya Abiria yaendayo Mikoani yakiwa yameegeshwa tu kwenye maeneo yake katika Kituo kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar.
Wakina mama hawa wakiwa wamemshikilia Mgonjwa wao waliekuwa wakimsafirisha kwente mkoani, wakiondoka stendi ya kuu ya Mabasi Ubungo baada kukosa usafiri kutokana na mgomo wa vyombo hiyo leo.
Hakuna shughuli yeyote inayofanyika Ubungo hivi sasa.
Mabasi yote yalikuwa tayari yamekaa mkao wa kuondoka, lakini mgomo ndio umekwamisha.
Abiria waliokuwa wasafiri leo kwenda mikoani wakiwa wamesimama bila kujua hatma ya safari yao.

Mabasi 
Hali ya Mgomo huu wa Mabasi umeleta hadha kubwa sana.

No comments: