Tuesday, April 14, 2015

TAMISEMI YATOA UFAFANUZI UHABA WA VYAKULA MASHULENI.

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu baadhi ya Shule za Sekondari za Bweni  zilizofungwa kutokana na ukosefu wa chakula ambapo alisema shule hizo zimefungwa kimakosa kwani Serikali imeshapeleka fedha za kununulia chakula kwenye halmashauri zote nchini. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba.
 Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Bw. Zuberi Samataba akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam mpango wa Serikali kuajiri waalimu wa shule za msingi wenye elimu ngazi ya Stashahada badala ya Cheti kama ilivyo sasa. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu ajira kwa walimu wapya waliohitimu 2014/2015 na kutoa rai kwa waalimu hao kwenda kuripoti kwenye vituo vya kazi watakavyopangiwa.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bw. Jumanne Sagini wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye ofisi za TAMISEMI  jijini Dar es Salaam. Picha na Fatma Salum (MAELEZO)

No comments: